Eliasi Mokiwa mwandishi anaedaiw kupigwa akiwa kazini na walinzi wa Gwajima
Mchungaji
Josephat Gwajima na wasaaidizi wake wameingia kwenye kashfa nzito ya
kumshambulia mwandishi wa habari Mkoani Tanga Ndugu Eliasi Mokiwa hadi
kumtengua kiuno chake kisa kikiwa kuwapiga picha misukule wake aliodai
kuwagomboa mikononi mwa wachawi wa Tanga.
Habari za
uhakika zilizothibitishwa na mwandishi wetu aliyekuwepo eneo ya tukio huko
Mkoani Tanga ambako Gwajima na wafuasi wake waolikuwa wakifanya hudia misukule.
Akizungumzia
tuki hilo mwandish huyo ambae anaripotia gazeti la Jibu la Maisha lakini ni
mwanafunzi wa chuo cha Royal College ngazi ya Cheti kilichopo Mkoani humo
alisema ilikuwa siku ya tarehe moja desemba 2013 saa kumi za jioni aliwa na
mwandishi wa gazeti hili Mkoani Tanga
Bwa Sadiki Amidu na wakiwa kwenye viwanja vya Tangamana wakati mchungaji
huyo akitangaza kuwa kuna msukule amedondoka katikati ya watu.
Mwandishi
huyo anasema alisogea na yeye ili kushuhudia msukule huyo pamoja na kumpiga
picha lakini katika hali isiyotarajia baada ya kupiga picha moja alishtuka
amepaishwa juu kumbe kuna msaidizi wa Gwajima ambae alimpiga mtama ulimpaisha
kimo cha ng’ombe na kudondoke kiuno.
Mara baada
ya kutua nchini mwandishi huyo anasema alisikia kitu flani kimelia kwenye kiuno
chake kumbe nyonga ilikuwa imeshateguka ambapo wakati akigragara chini walikuwa
wasaidiz wanne na walimbeba juu hadi nyuma ya jukwaa na kuanza kumsurubu,
wakati huo Mchungaji Gwajima alikuwa anashuhudia mchezo mzima bila kutoa kauri
yeyote.
Mwandishi
huyo aliendelea kueleza “ Nilipigwa sana huku wakinisachi mifukoni na
kunichukulia pesa yangu yote ambayo ilikuwa ni shilingi elfu tano ya nauli huku
wengine wakiniuliza kama pesa nyingine nimeweka wapi lakini kiwajibu kuwa sina
pesa nyingine na kuwaeleza mimi ni mwandishi wa habari hivyo wasinidhalilishe
kiasi hicho lakini hawakutaka kusikia” Alisema Eliasi
Hata hivyo
Eliasi aliendelea kusema kuwa “ Mwandishi mwezangu baada ya kuona vile alitimua
mbio kuokoa maisha yake kwani walishashtukia kuwa tuko wawili hivyo huenda
wangetukamata wote, baadae alikuwa mchungaji mmoja mwanamke ambae sikufahamu
labda huenda alikuwa mke wa Gwajima kutokana na heshima waliyompa muda ule
kwani wakiwa bado wananishambulia kwa ngumi za chembe na walipomuona mama huyo
waliniacha haraka na kuganda” Alisema mwandishi huyo
Baada ya
mama huyo kuuliza kosa langu nini wakamueleza kuwa kuwa mimi nimepiga picha
misukule na nilikuwa navizia watu waliokaa uchi na kuwapiga pamoja na misukule
yao, ambapo mama huyo aliamuru niachiwe huru lakini kama hizo picha za misukule
zipo kwenye kamera yangu zifutwe halafu wanirusu na mama huyo aliangalia kwenye
kamera na kukuta hamna picha yoyote ya aina hiyo.
Hata
hivyo Eliasi aliendelea kusema
“Nilivyoachiwa huku nikiwa nyang’anyang’a nilijisogeza kidogo kidoga hadi kituo
kikuu cha Polisi na kutoa taarifa na wakampatia Jarada la Upelelezi PE namba 71
-2013 pamoja PF3 ambapo alikwenda kwenye Hospitali ya Jiji ambako walimpatia
matibabu hadi siku iliyofuta ambapo alirudi na ile PF3 tena Polisi.
Aidha
kutokana na mkutano huo kuwa isku ya mwisho kwenye viwanja hivyo na wakahitaji
kuongeza siku za mkutano lakini walizuiwa kibari badara yake walihamishia
mkutano huo kwenye viwanja vya Ridochi.
Na baada ya siku mbili Polisi wakiwa na Deffender walikwenda kuvamia mkutano
huo kwa lengo la kuwakamata wale wote walihusika na tukio la kumpiga na
kujeruhi mwandishi huyo, lakini kwa bahati mbaya mwandishi huyo akiwa
ameandamana na Askari hakuwata wale walimpiga hivyo na kufanya Polisi kuendelea
na uchunguzi wa tukio hilo.
Baada ya
taarifa hizo Maskani Bongo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga “RPC” Masawe ili
kuzungumzia ishu hiyo ambapo alipatikana lakini kwa bahati mbaya akajibu kuwa
yuko kwenye mafunzo Moshi hiyo tumtafute Kaimu wake ambae nae alipopigiwa simu
simu hiyo iliita tu bila kupokelewa.
Misukule ya
mchungaji Gwajima imekuwa na utata mkubwa sana kwenye jamii kutokana na wengi
kuamini kuwa ni propaganda tu za kujizolea waumini, kwa mfano misukule wote
aliowatoa Mkoani Tanga wanadaiwa ni wa kutengenezwa ndiyo maana amekuwa mkali
kwa waandishi ili wasije kuripoti uwongo huo.
Hata hivyo
kwa wakazi mji wa Tanga wamesikitishwa
na tukio hilo na kupigwa kwa mwandishi huyo maarufu ambae ni ndugu moja na
mtangazaji wa TBC1 Domonic Mokiwa.
No comments:
Post a Comment