TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, August 24, 2013

CUF WACHARUKA WAMWAMBIA NCHIMBI KAMA ASIPOWAKAMATA WAUZA MADAWA YA KULEVYA AJIUZULI!



Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
Baraza kuu la uongozi wa Taifa la Chama cha Wananchi (CUF), linamtaka Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,  Dk. Emmanuel Nchimbi kujiuzulu kama atashindwa kuwakamata na kuwawajibisha matajiri wakubwa wanaofadhili mitandao ya biashara ya  madawa ya kulevya.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati akielezea maazimio yaliyoamuriwa na kikao cha  Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho.

Profesa Lipumba alisema kuwa anampongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kubeba majukumu yaliyotakiwa yafanywe na Waziri wa Mambo ya Ndani  ya Nchi.

Waziri Mwakyembe ana majukumu mazito ya kusimamia reli, bandari na viwanja vya ndege, usafirishaji na uchukuzi na kusikitishwa na uzembe unaofanywa na Jeshi la Polisi chini ya usimamizi wa mambo ya ndani kwa kushindwa kusimamia na kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya,” alisema.

Alisema bila aibu serikali inachukua hatua ya kumfukuza kazi askari polisi mwenye cheo cha koplo kwa kusaidia kupitisha madawa bila kuzingatia ukweli, na kudai kuwa koplo huyo alitumwa na vigogo kutoka serikalini.

“Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ipambane na mapapa wa utoroshaji wa nyaraka za serikali na madawa ya kulevya badala ya kufanya geresha ya kupambana na vidagaa wa biashara hizi ambazo hata wakichukuliwa hatua kali bado wakubwa wa biashara hii wanaendelea kuliangamiza taifa,” alisema.

Aidha, alisema  Baraza Kuu  linamtaka Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, ajiuzulu kwa uzembe wa kupigwa risasi Sheikh Ponda Issa Ponda na pia kupisha uchunguzi wa tukio hilo na kama hatafanya hivyo, serikali imwajibishe kwa lazima.

Aliongeza kuwa baraza linalaani kitendo cha kikatili cha kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda.

“Sheikh huyu alipigwa risasi bila sababu, kwani hakuwa akipambana na polisi na wala hakuwa na silaha yoyote, hivyo baraza linaitaka serikali kuunda tume huru itakayochunguza suala hili kama zilivyoundwa tume huru nyingine kwenye matukio kadhaa ya uvunjwaji wa haki za binadamu.”

Aliongeza kuwa baraza linasikitishwa na kufedheheshwa na mgogoro wa kiuchumi uliotangazwa na nchi jirani za Rwanda na Uganda kuhusu kutotumia Bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya ubabaishaji unaofanywa na vyombo vya dola kama vile jeshi la polisi na askari wa usalama barabarani.

Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutafuta njia za kidiplomasia ili kuweza kutatua mgogoro wa kisiasa baina ya Tanzania na Rwanda ili kuleta maelewano ambayo yatadumisha mahusiano na usalama baina ya nchi hizi
.

No comments:

Post a Comment