TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, April 5, 2013

WATAZAMAJI WA DTV WALA SHAVU NONO, KUJIZOLEA VING'AMUZI, FLAT TV BUREEEEEEEEEE!

Na Livingstone Mkoi

Katika hali ya kuonesha upendo na kuwajali watazamaji wake kituo cha televisheni cha Dar Es Salaam Televishen 'DTV' kimeandaa programu maalum ya kuwapatia zawadi kem kem watazamaji wake ambazo zitakuwa zikitolewa kila siku.

Akiongea na Xdeejayz mratibu wa programu hiyo Bravo P Mathew alisema" Tumeamua kurudisha fadhira kwa mashabiki wetu ambapo hapa tumelenga watazamaji wa DTV, wasikilizaji wa Magic Fm na Times Fm ambapo kila siku watakuwa wanajishindia zawadi rukuki za viang'amuzi na Flat TV" Alisema mratibu huyo

Aidha Bravo aliongeza kusema kuwa watazamaji wa DTV na wasikilizaji wa Times na Magic wanapaswa kusikiliza  vituo hivyo ili kupata taarifa mbalimbali za ushindaji huo. Ambapo ili kuwa mshiriki unatakiwa kutuma neno SHINDA kwenda namba  15522 na hapo kutakuwa na maswali kadhaa rahisi kisha unaweza kujishindia zawadi hizo.

Bravo alitoa hamasa kwa mashabiki hao kwani hii ni nafasi nzuri kwao hivyo waichangamkie haraka ili wajizolee zawadi hizo kibao hii mtu mmoja anaweza kujing'akulia zaidi ya mara mbili itatokana na jinsi atakavyokuwa anashiriki.

No comments:

Post a Comment