TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, April 5, 2013

ELEPHANT MAN AZIKUMBUKA CHIPSI MAYAI ZA BONGO!


Na Livingstone Mkoi kwa msaada wa mtandao

Mwamuziki mwenye jina kubwa ulimwenguni ambae mwaka juzi alikuwepo nchini na kufanya show ya kufa mtu kwenye fukwe ya Mbaramwezi na kuzikonga nyoyo za mashabiki Elephant Man ameibuka na kusema kuwa kwenye ziara zake barani afrika kamwe hawezi kuisahau Tanzania kwani kikubwa kinachomfanya aikumbuke bongo ni chakula maarufu cha Chipsi Mayai ambacho alitokea kikipenda sana.

Akiongea kwenye mtandao huo maarufu nchini Jamaika wa Reggaehall Elephant alisema kutumia lugha ya kijamaika ya Patwa alisema na hapa imetafisiliawa kiswahili" Guys nimekumbuka chakula kimoja kipo nchini Tanzania kinaitwa chipsi mayai ni kitamu sana.... na kama nikijairiwa kurudi tena Tanzania nitakinunua cha kutosha na nitakuleteeni watu wangu mkione" Alimaliza kusema mwanamuziki huyo huku akipewa koment kibao.

Mwanamuziki huyo ambae kipindialichokuja alifikia kwenye Hotel ya Colosseum iliyopo Masaki Jijini Dar na alipendelea sana kula chipsi mayai baada ya kuonja chakula hicho hakula chakula chochote kingine hadi anaondoka nchini.

No comments:

Post a Comment