Mwanamuziki 20% Pacent
Na Livingstone Mkoi
Baba mzazi wa mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Abasi Kizansa (20% Pacent) mzee Kizansa inadaiwa hali yake sio nzuri kutokana na upasuaji aliofanyia hivi karibuni.
Akiongea na xdeejayz kwa sharti la kutotajwa jina lake mmoja wa wadogo wa mwanamuziki huyo alisema kuwa baba yao hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa tumbo kwa maradhi ambayo hakuyataja.
Hata hivyo hadi jana Jumatano usiku kulikuwa na taarifa kuwa mzee huyo anaeishi Kimanzi alizidiwa na kurudishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Xdeejayz ilimtafuta mwanamuziki huyo kupitia simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia zaidi taarifa hizo lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana.
No comments:
Post a Comment