MABINGWA wa Kombe la Kagame Yanga, jana wamefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia nchini (TBL), kilichopo Ilala jijini Dae es Salaam, ambacho kinaidhanmini klabu hiyo kupitia bia ya Kilmanjaro.
Akiongea katika ziara hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake iliamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho, ili kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinwaji mbali mbali, ikiwamo Kilimanjaro.
Alisema kuwa, Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimichezo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa, na kwamba wamefurahishwa na aina ya mapokezi waliyoyapata kiwandani hapo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.
"Tunawaomba muendele na moyo huo huo kwani sisi kama Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanikio ya klabu yetu kwa sasa na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, na kwamba kwa pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora," alisema Sendeu.
Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo cha Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao, kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.
Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager inathamini mchango wa timu ya Yanga katika maendeleo ya soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hiyo, huku akibainisha kuwa wataendela kuidhamini kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.
Thamani ya udhamini wa Kilimanjaro kwa Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni (Shillingi Bilioni mbili za Kitanzania) kwa mwaka. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya shughuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wa kimataifa, mabasi, vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka.
"Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa Yanga imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia timu yao.
"Ushirikiano wetu na Yanga unatokana na ukweli kwamba, ni kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini," alisema Kavishe
Nizaa alfani na canavaro wakipita kutembelea kiwanda cha tbl
Maelekezo yanatolewa kukijua zaidi kiwanda cha bia na jinsi bia inavyotengenezwa
Ilikuwa ni makuku na bia mwanzo mwisho
msosi wa nguvu ulihusika sana siku hiyo
mstari ukaanza
picha ya pamoja ya wafanyakazi na viongozi wa tbl na wachezaji na viongozi wa yangaMashabi namba moja wa yanga hemed kavu (hk),petit man wakuache na shabaha the don wakiwa uwanjani katika kombe la kagame mechi kati ya azam na yanga, azam ililala 2-1
No comments:
Post a Comment