TANGAZO MAALUM
TANGAZA NA SISI
Wednesday, September 5, 2012
KIBOMU CHA LEO
KUNA JAMAA ALIENDA KUPOSA KWA MZEE MMOJA ILIKUWA HIVI!!!
MZEE: Yaani wewe Umekuja kuposa huku Unatafuna Big G? Si Dharau hiyo!!
JAMAA: Natoa Harufu ya Sigara Mzee..
MZEE: Unasemaje? Unavuta Sigara Pia?
JAMAA: Nikitoka Club kulewa ndio huwa navuta Sigara Mzee..
MZEE: Tobaa! Unalewa Pia!?
JAMAA: Nilianza Kulewa Nilipokuwa Jela...
MZEE: Yaani na kufungwa pia umeshawahi?
JAMAA: Ahh Si Niliuwa Mtu.
MZEE: Mtumeeee!!!! Kumbe wewe muuaji!!!! Astaghafillulah..
JAMAA: Si Kuna mzee mmoja bwege nilitaka kumposa mwanae akanikatalia, Si nikamuulia mbali
MZEE: Karibu Baba, Unataka harusi lini? Mimi Sina tabu, Mke tu Umepata!! Mkeo huyu hapa, kazi kwako baba..
....HAHAHAHAHAHAHAHAAAA ... comment kama umeipenda... By mau
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment