ANGALIA PICHA ZA RAIS UHURU KENYATA ALIVYOSIMAMISHA GARI NA KULUA CHAKULA KWA MAMA NTILIE NA KUNYWA MAJI YA KANDORO HII HAIJAWAHI TOKE KWA MARAIS EAST AFRIKA. XDEEJAYZ LIVE..!
Vituko vya mara kwa mara haviishi kwa Raisi
wa Kenya, Bwana Uhuru Kenyata, ambapo wiki hii wakati alipotoka kwenye mkutano
wake yeye na marais wengine aliamua kusimamisha msafara wake na kupata chakula
cha mchana eneo la kawaida kabisa.
Tukio hilo limewashangaza wengi ambao
walikuwa wakishangaa msafara huo wa Rais ukipita mara ghafla ukakata kona na
kupaki pembeni na waheshimiwa kushuka kupata mlo wao wa mchana kwenye eneo
liitwalo Kaijado tena chini ya mti. Walioshuka kupata chakula cha mchana ni Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto pamoja na wasaidizi
wao.
Rais Kenyatta anaonekana kuwa karibu na
kutaka kuishi maisha ya kawaida tofauti na yale ya waheshimiwa maraisi wa nchi zingine,
ambapo wiki iliyopita video moja ilimuonyesha akinunua karanga kwa muuzaji
anayetembeza mtaani.
Hakuishia hapo pia aliwahi kutembea jijini Nairobi bila msafara kama
ilivyozoeleka hadi Trafiki akamshangaa aliporuhusu gari za upande huo na
kumuona akiwa anaendesha gari hizo ambazo alizisimamisha kwa muda kidogo.
No comments:
Post a Comment