Pages

Tuesday, December 3, 2013

HAYA NDIYO MAAJABU YA KAZI YANGU YA WHO’S BAD: MTUNISY.



MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu Swahiliwood Nice Mohamed ‘Mtunis’ ametamba kwamba filamu yake ya Who is Bad itakuwa kazi yake ya kufungia mwaka kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na sinema hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi karibuni.
“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who is Bad itafunga mwaka kama kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.
Sinema hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki wengine wanaofanya katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Mtunis amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama Bar mead, Who is Bad na kusambazwa  na kampuni ya Steps Entertainment.

GAZETI LA MASKANI BONGO LITAKUWA MTAANI WIKI IJAYO TAREHE 11 DESEMBA DAKA KOPI YAKO MAPEMA!

No comments:

Post a Comment