Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita  kwamba kama 
ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye  atafurahi sana  
kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa.
" Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo.
"Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa 
Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata  wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO 
Rais  akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi," 
amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.
"ZUNGU MNYAMA AWAAHIDI MAKUBWA WAKAZI WA MOROGO KWENYE UZINDUZI WA CLUB MAISHA NI TAREHE 19-20 MWEZI HUU" 

No comments:
Post a Comment