Pages

Monday, July 22, 2013

MTALAKA WA HAMMER Q AMPA ONYO KALI MKE WA MWIMBAJI HUYO, AMWAMBIA NDOA SIO SAWA NA KUIMBA TAARABU!

 Yasmeen Yakubu ambae ni mtalaka wa mwanamuziki nyota nchini Hammer Q.

 Mwanamitindo mahali nchini Yasmeen Yakubu.
 Yasmeen Yakubu amemjibu mke wa aliyekuwa mumewe wa zamani Hammer Q, Salha Abdala kuwa aache kumtafuta mchawi anaeivuruga ndoa yake badala yake aangalie ndo yake kwani ndoa sio kama kuimba taarabu bali ni kazi ngumu sana.
Mke wa Hammer Q Salha Abdalah.



 Mwimbaji wa kundi la Dar M Taarab Salha Abdala akiwa na bandeji kichwani baada ya kujeruhiwa vibaya na mumewe Hammer Q hivi karibuni katika ugomvi ambao mwimbaji huyo alisema ulisabaisha na mtalaka mwenzake Yasmeen Yakubu


Hammer Q.

 Na Livingstone Mkoi
Aliyekuwa mtalaka wa mwanamuziki nyota wa taarabu nchini Hammer Q aitwae Yasmeen Yakubu ameibuka na kumpa onyo kali mke wa sasa wa mumewe huyo wa zamani na kusema aache kumtafuta mchawi wa ndoa yake kwani ndo sio kama kuimba taarabu bali inahitaji kutulia.

Akiongea ndani ya ofisini za Xdeejayz hivi karibuni Yasmeen alisema hayo baada ya mke huyo wa Hammer Q ambae pia ni muimbaji wa kundi la Dar modern Taarab kumtuhumua kuwa yeye ndiye chanzo kupigwa nusra ya kutolewa nafasi na mumewe.

Yasmeen aliendelea kuieleza Xdeejayz alikuwa wiki iliyopita alikuwa nje ya nchi alisikia taarifa toka kwa watu wake wa karibu kuwa Salha alikuwa nahojiwa na kituo kimoja cha radio ndipo aliomtuhumua mke mwenza huo kuwa ana mahusiano na mumewe.
Mwanamitindi huyo alisema kuwa alishtushwa sana na taarifa hizo kwani yeye tangu ameachana na Hammer miaka mitano iliyopita hajawahi kukutananae kwa njia yoyote ile" Hivyo jamani namshauri tena huyo mwanamke akae chini ili kujua tatizo anakosea wapi ili ajirekebishe ili asipigwe tena na sio kukurupuka na kuanza kupakazia watu, mimi naishi na mchumbaangu na familia yangu hivyo sielewi tuhuma anazonipakazia huyo mwanamke zinatoka wapi" Alimaliza kusema Yasmeen


No comments:

Post a Comment