Huyu ni mmojwa aliyekuwa baunsa maaarufu aliyefahamika kwa jina la CHURA kabla ya kufikwa na umauti akiwa Hospital ya Mwananyamala baada ya kukatwa katwa mapanga kichwani eneo la tukio.
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Wakazi zaidi ya elfu 5000 wa kata ya Wazo mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa juzi walifanya kumbukumbu ya kuwakumbuka marehemu wote waliorafiki kwenye migogoro ya ardhi kwenye mtaa huo huku wananchi hao wakimuhusisha Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kuwa kama angekuwa tayari mkuu wa Wilaya basi mauaji hayo yasingetokea leo hii.
Wakiongea na mtandao huu wa habari za uchunguzi wananchi hao walisema " Kiukweli tunawakumbuka ndugu zetu waliopoteza maisha wakiwemo wale mabaunsa waliopigwa mishare ya kichwa na mapanga kisa mgogoro huu wa ardhi ambao kwa sasa Mheshimiwa Makonda anakwenda kuumaliza na tunaamini kama Mheshimiwa Makonda angekuwepo hakika hakuna tone la damu ambalo lingemwagika" Walisema
Hata hivyo wananchi hao wameendelea kumuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kumuongezea majukumu DC Makonda kwa kumpa ukuu wa Mkoa kwani kwa sasa ndiye DC pekee anaefanya kazi usiku na mchana huku mafanikio yake yakionekana hali inayopelekea hata Wilaya nyingine za Jiji la Dar wakihitaji msaada wake.
Hata hivyo licha ya zoezi la uhakiki kubakisha wiki mbili kumalizika, lakini kwa sasa limesimama kidogo kufutia kuwepo kwa mtafaruku wa kati ya mtu aliyedai kuwa hilo shamba lake ambae ilifahamika kama alishaliuza kwa muhindi huku RC na DC Lugimbana wakidaiwa kuwa mashahidi wa mauziano hayo, hivyo kwa sasa eneo hilo lipo chini ya muhindi lakini cha kushangaza muhindi amegoma kujitokeza badara yake amekuja mtu aliyeuza tayari eneo hilo huku kamati za ardhi kata hiyo zikifahamu fika kama huyo mtu eneo hilo halimuhusu tena.
Aidha wakazi hao ambao wengi wao ni wakina mama wanasema wanampango wa kufanya sherehe kubwa ya kumpongeza DC Makonda kwa kazi nzuri ya kutenda haki aliyoifanya bila kuogopa nguvu ya mafisadi lakini pamoja na kigogo mwenye mamlaka kuliko yeye ambae anadaiwa kwenye mgogoro huo anamkono wake.
TANGAZO MAALUM
.
TANGAZA NA SISI
Wednesday, February 10, 2016
Sunday, February 7, 2016
ANGALIA MECHI YAKE YA KWANZA YA MBWANA SAMATTA AKIWA NA KRC GENK YA UBELGIJI...!
Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea tena leo February 6 kwa michezo kadhaa kupigwa, miongoni mwa michezo iliyochezwa leo February 6 ni mchezo kati ya Mouscron FC dhidi ya klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, mchezo huu ulikuwa na mvuto kwa Tanzania zaidi kwani ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta kucheza toka amejiunga na klabu hiyo.

Mbwana Samatta ambaye ndio nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya KRC Genk akitokea benchi, Samatta aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis ambaye alitoa pasi ya goli la ushindi kwa KRC Genk dakika ya 63 na Thomas Buffel kupachika mpira nyavuni.

Mchezo ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji wao Mouscron, lakini hadi mpira unamalizika Mouscron walikuwa wanaoongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 53 na KRC Genk asilimia 47, ushindi huo umeifanya KRC Genk kutimiza jumla ya point 38 na kusogea hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi. KRC Genk wanarudi tena dimbani February 13 kucheza dhidi ya Waasland-Beveren katka dimba lao la Cristal Arena.

Saturday, February 6, 2016
UKAWA DAR WAMPIGIA SALUT DC MAKONDA, WAMTAKA AGOMBEE UBUNGE KUPITIA CHAMA CHOCHOTE WATAMPIGIA KURA ZA KUMWAGA, MASKANIBONGOTZ INASHUKA NAYO.....!
DC MAKONDA KATIKATI AKIWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA MH MBOWE HIVI KARIBUNI KWENYE MAJUKUMU YA KITAIFA.
Na Mwandisahi wa Maskanibongotz
Wafuasi wengi wa Ukawa Kinondoni Jijini Dar wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na ufisadi na kuwa mtetezi wa wanyonge hasa kwenye suara la migogoro ya
ardhi.
Wakiongea na maskanibongotz wafuasi hao walianza kusema kuwa" Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Makonda ni kiongozi anaehitajika kwa watanzania na hata hivyo sijui kwa nini mheshimiwa Rais alichelewa kumteua huenda hata watu wasingepoteza maisha kule Nyakasangwe" Walisema watu hao
Hata hivyo wananchi hao waliongeza kusema kuwa Makonda angepewa Ukuu wa Mkoa wa Dar ili amalize matatizo ya ardhi kabisa kwani hata wilaya nyingine za Jiji la Dar zinamuhitaji kwani alichokifanya Wazo kwenye mtaa wa Nyakasangwe hakika anastahiri pongezi ikizingatia viongozi wengi akiwemo Mkuu wa Mkoa Meck Sadick walishindwa kumaliza tatizo hilo.
Aidha wananchi mbalimbali walitamani hata DC huyo kugombea ubunge Jimbo la Kawe ama Kinondoni ili akapaze sauti yake bungeni.

Friday, February 5, 2016
AFANDE MACHEMBA AWAAMSHA USINGIZINI RAY NA JB, MASHABIKI BONGO MOVIE WAWATAKA MASTAA HAO KUSTAAFU SANA KUPISHA DAMU CHANGA...!
AFANDE MACHEMBA
WASANII WENYE MAJINA NCHINI TANZANIA BONGO MOVIES TEAM
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Kipaji cha Msanii kinda kwenye tasnia ya Filamu Tanzania
Joseph Machemba sasa kimeonekana kuwaamsha uzingizini mastaa wa kiume Vicent
Kigosi"Ray" Na Jakobu Steven "JB" na wengine huku mashabiki
wengi wakiwashauri Ray na Jb kuachana na sanaa kwa sasa.
Mashabiki hao wakiongea na maskanibongotz walisema kwa kipaji
anachokionesha msanii Afande Machemba
hakika ni dhahiri kabisa anaweza kuifikisha sanaa ya Tanzania Kimataifa
na sio kama Ray na Jb ambao kwa sasa wanasafiria nyota za zamani kwa kushindwa
kufanya juhudi zozote za kuwa wa kimataifa.
Mashabiki hao waliendelea kusema wamefurahishwa na upinzani
mkali aliouonesha Afande Machemba kwenye
sanaa kwani kulizika kwa msataa walipo kungeweza kuleta athari kwenye sanaa hii
kwani Ray na Jb uwezo wao ulishakufa tangu alipotangulia mbele za haki Marehemu
Steven Kanumba hadi leo sanaa ya Filamu imerudi nyuma kwani hakuna hata staa
mmoja ambae anaonekana ana kiu kama aliyokuwa nayo marehemu Kanumba ya kuifika
sanaa ya Tanzania kimataifa.
Filamu zilizomtambulisha Afande Machemba ni Filamu
alizoonekana Afande Machemba ni pamoja na, Karoge Tena, Night Dress, Akiri Nyingi, Bifu
la Kitongoji na ndani yake ameonesha kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwafanya
mashabiki wanajiuliza kwa nini alikuwa amechelewa kuanza kuigiza.
Thursday, February 4, 2016
MUNGU AZIDI KUONESHA MAAJABU YAKE NDANI YA KANISA LA MCHUNGAJI MWENYE NGUVU YA KIPEKEE, MAMIA YA WATU WAZIDI KUMIMINIKA , WAGONJWA WA UKIMWI, WASIOPATA WATOTO SASA WABEBA MIMBA, NI MAMBO YA KUSHANGAZA KWELI..!
Hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Kanisa la Sayuni lililopo Nyakasangwe Kata ya Wazo, ambapo kutokana na uponyaji wa kweli unatendeka Kanisani hapo mamia kwa mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi ili kupata uponyaji wa kweli. Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Mzola ameendelea kuwataka watanzania kuendelea kufika Kanisani hapo kwa ajiri ya kupata uponyaji wa papo kwa hapo.
Mrs Mzola akiwa kwenye ibada
Ndani ya Kanisa hilo uponyaji hufanyika wa papo kwa hapo bure bila malipo
Mchungaji Mzola
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Katika hali ya kushtua baada ya kuvuja kwa taarifa za Kanisa linalotibu mardhi ya aina yote huku Mungu akimtumia mtumishi wake Mch Mazola kufanya hayo yote maelfu ya watu wameendelea kumiminika Kanisani hapo kiasi cha kukosekana nafasi ya kukaa kwa ajiri ya kupata uponyaji wa bure.
Mchungaji huyo akiongea na gazeti la Maskani Bongo alisema" Kiukweli tunamshukuru Mungu Muumba mbingu na ardhi kwa baraka zake toka habari ziwafikie watu wake basi wamekuwa wakimiminika usiku na mchanga kuja kupata uponyaji wa kweli" Alisema mchungaji huyo
Mchungaji huyo aliongeza kusema kuwa anaendelea kutoa uwito kwa watanzania wote kuendelea kufika Kanisani kwake ili wapate uponyaji, kwani Kwa Mungu hakuna lisilowezekana, kila magonjwa yote sugu, ugumba, utasa, mikosi ya kushindwa kuolewa/kuona, kuwa na mashaka, hofu ya kifo nk.
Na amesema watkaoshindwa kufika kanisani kwake Kata ya Wazo mtaa Nyakasangwe wanaweza kumpigia simu kupitia namba hizi 0763-161785/ 0713-161785 na wao watapokea uponyaji huko walipo.

Thursday, January 28, 2016
AFANDE MACHEMBA AWATOA MACHOZI KWA UCHUNGU WAKAZI WA KANDA YA ZIWA, WASEMA KIPAJI ANACHOKIONESHA WANAKUMBUKA MAREHEMU STEVEN KANUMBA ALIVYOWEZA KUITANGAZA NCHI KIMATAIFA..!
Afande Machemba katika ubora wake akiwa kwenye picha ya pozi dakika chache kabla ya kuingia Location kukamua kwenye moja ya filamu alizoshirkishwa hivi karibuni huko Mkoani Arusha mara baada ya kupokea mwaliko toka kwa wasanii wa huko wakimtaka akacheze filamu.
Afande Machemba
Marehemu Steven Kanumba ambae ni kabila moja na Afande Machemba wote ni Wasukuma.
Na Mwandishi Wetu-Mwanza
Msanii Kinda toka kiwanda cha filamu za Kitanzania Joseph Machemba ameendelea kuwa gumzo nchini na safari hii mashabiki wa filamu toka Kanda ya Ziwa wamejikuta wakibubujikwa na machozi mara wanapoongalia filamu alizocheza msanii huyo toka Shinyanga ambae kwa sasa amehamishia makazi yake Jijini Dar huku wengi wakimfananisha na Marehemu Kanumba.
Mmoja wa wadau wa filamu Mkoani Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Majiha Mankunga alisema' Jamani tunamshukuru Mungu kwa kutupoza machungu tuliyoyapata miaka kadhaa iliyopita kwa kuturudishia mtu mwingine muhimu kwetu, huyu Afande Machemba hakika ni kama Kanumba amezaliwa upy" Alisema mtu huyo ammbae ni msambazaji wa filamu za kitanzania kanda ya ziwa
Msanii Joseph Machemba ambae kwa sasa anatamba kwenye filamu za Bifu la Kitongoji na Filamu ya AKIRI NYINGI ambazo ndani yake msanii huyo ameonesha uwezo wa ajabu kiasi cha kuwashangaza mastaa mbalimbali wa bongo movie kwa kipaji alichokuwa nacho Afande Machemba, Huku watanzania wengi wakimtakia kila raheli msanii huyo kwa juhudi zake

Saturday, January 23, 2016
WACHUNGAJI, MASHEKH WAWACHARUKIA RAIS MAGUFULI, DC MAKONDA NA LUKUVI, WAFUNGA SIKU 40, WASEMA MUNGU ATAKACHOWAFANYIA ULIMWENGU UTAJUA...!
Mmoja wa wazee wa Kanisa la Hossana akiwa kwenye hisia kali ya maombi kwa Mungu
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Hosana Mch Mzola
Waziri wa Ardhi Mh Lukuvu kwa sasa yupo chini ya maombi hayo ili afanye maamuzi sahihi.
Mchungaji Amos Mbena Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Holness Mision lililopo Kimara lakini mchungaji huyo amekuwa akiguswa sana na mgogoro huo hivyo nae ameungana kuongeza nguvu ya maombi ili viongozi hao wasikie kilio cha wananchi hao.
Shkhe Sharif Khamis kijana mwenye nguvu ya ajabu kwenye maombi nae ameungana na watumishi hao mbalimbali na wananchi kwenye maombi ya kumaliza mgogoro wa ardhi wa eneo hilo.
Wakina mama na watoto ambao kwa sasa wanaishi mazingira magumu baada ya nyumba zao kubomolewa na polisi kwa shinikizo la mafisadi, wakimlilia Mungu wao.
Na Mwandishi wa Maskanibongo Gazeti
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda, Rais Magufuli na waziri wa Ardhi Mheshimiwa Lukuvu wapo chini ya maombi makali ya siku 40.
Wakazi wa Kata ya Wazo kwenye Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wakishirikiana na mashekh na wachungaji wameanzisha maombi hayo maalum kwa ajiri ya Mungu kuwafungua viongozi hao ili wamalize mgogoro huo ndani yake wenye harufu ya rushwa na ufisadi huku maafisa Ardhi na watu wa Mipango Miji Manspaa ya Kinondoni wakitajwa kuhusika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wachungaji wa makanisa yaliyopo Mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa walisema" Tupo kwenye maombo haya ili Mungu awafungue viongozi wetu kwa vile wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho wamalize hili jambao kwani tunaamini Tanzania kwa sasa imepata rais ambae watanzania walikuwa wakimuhitaji hivyo tumeona ni vyema tukamlilia Mungu azidi kumfungua zaidi na kuona hata mgogoro uliopo kwenye mtaa wetu " Alisema Mchungaji Mzola
Hata hivyo wachungaji hao waliendelea kusema kuwa kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Paul Makonda ni kubwa sana na hakika sasa mahara alipofikia anahitaji nguvu ya maamuzi ya Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Rais kwa vile mtandao alioukuta mheshimiwa Makonda kwenye mgogoro wetu ni mkubwa na inaelezwa ndani yake kuna baadhi ya vigogo wa Ardhi Manspaa.
Wakazi hao waliendelea kusema Mheshimiwa Makonda amediliki kuhatarisha maisha yake kwa kupigania haki ya wananchi licha ya kwamba amekuwa akikutana na vikwazo kutokana na kuzungukwa na watu ambao hawapo upande wake bali wakiwa upande wa mafisadi hivyo sasa ni zamu ya Waziri kumpa meno ya yenye makali kumaliza mgogoro huo kwa kutoa maamuzi yatakayoondoa kabila mgogoro huo.
Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa inaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Bilebela ambae amekuwa kipenzi cha wakazi hao kutokana na utendaji wake wa hali na kuogpa rushwa kama ukoma, hali hiyo imepelekea kuchukiwa na upande wa pili wa mafisaidi kiasi cha kumtengenezea zengwe kila kukicha kwa kutumia pesa waliyokuwa nayo
Subscribe to:
Posts (Atom)