TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, June 24, 2014

Goodnews Kwa mara ya kwanza ndege ya @fastjet yarushwa na maarubani Watanzania.


Fastjeta mimi
Jina la fastjet sio geni Tanzania na hii ni kutokana na kuzidi kukua kila siku kutokana na huduma inayotolewa kusafirisha abiria kutoka kona kadhaa za Tanzania kwa kuzingatia muda na bei nafuu pia.
Good news ni kwamba shirika hili la ndege ambalo limekua likisafirisha abiria wa ndani ya nchi kati ya Dar es salaam na Mwanza,  Mbeya na Kilimanjaro kwa sasa, limeanza kuwapa shavu marubani Watanzania.
Kwa mara ya kwanza Marubani Watanzania Arif Jinah na William Zelothe wameirusha ndege ya abiria ya Fastjet A319 mpaka Mwanza wakiwa wamezingatia viwango vya usafirishaji vya kimataifa ambapo marubani hawa wako kwenye idadi ya Marubani zaidi ya kumi Watanzania walioajiriwa na fastjet.
Siku zote wafanyakazi ndani ya ndege na kwenye ofisi zao ni Watanzania kwa asilimia kubwa ila Marubani ndio hawakuwa Watanzania.
Unaambiwa fastjet ilipoanza kufanya kazi Tanzania ilikosa marubani wanaoweza kuendesha ndege aina ya Airbus na ndio maana hii ni good news manake Watanzania wa kwanza wameweza kufuzu na kuendesha ndege wao wenyewe.
Hongera sana kwa rubani Arif Jinah na William Zelothe.
Fastjet 2
 Millard Ayo, mkali wa bongofleva Ommy Dimpoz na Mohamed wa fastjet tukiwa kwenye ndege ya fastjet kuelekea Johannesburg South Africa.
Kwenye sentensi nyingine nimeona nikuachie na hii good news nyingine ya Fastjet kuanza kusafirisha abiria kati ya Dar es salaam mpaka Harare August 5 2014 ambapo wataanzia kwa safari mbili kwa wiki.
Safari ya fastjet kati ya Zimbabwe na Tanzania inakua ya tatu kimataifa huku nyingine zikiwa ni kati ya Dar es salaam na Johanesburg South Africa pamoja na safari ya Lusaka Zambia huku zikiwa ni safari za bei ndogo kabisa pale abiria anapowahi kufanya booking.
Unawazungumziaje fastjet mtu wangu? umeonaje shavu walilowapa Watanzania?

Marufuku ya Mahakama kuhusu neno ‘Allah’ kutumiwa na gazeti

Screen Shot 2014-06-24 at 7.23.55 AMHii ni moja kati ya zile kesi za kanisa katoliki zilizodumu kwa muda mrefu sana manake hii ilianza toka mwaka 2007 pale ambapo serikali ya nchi hii ilitishia kulifungia gazeti la kanisa hili kama lingeendelea kumuita Mungu Allah.
Taarifa mpya ya sasa inasema Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa katoliki nchini humo kumuita Mungu ‘Allah’ kwenye gazeti hili linaloandika habari zake kwa lugha ya Ki malay.
Walidai kuwa Wakristo wanawakanganya Waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa ambapo uamuzi wa Mahakama ni mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria za kanisa katoliki zilizochukua muda wa miaka saba na kusababisha mashambulizi katika makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh mwaka 2010.
Screen Shot 2014-06-24 at 7.29.55 AM 
BBC wanaripoti zaidi kwamba Wakristo na wasikh wanadai kuwa wamekuwa wakimwita Mungu ‘Allah’ katika lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda mrefu sana.
Mahakama nayo imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa katika ukristo ambapo mgongano huu kuhusu neno hilo moja umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofautitofauti lilivyogawanyika.
Wanaharakati wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya Mahakama huku wengi wao wakiwa wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu ‘Allah’ kama njia ya kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo wamekana.

NAKAAYA AMUANIKA MTOTO WAKE HADHARANI YADAIWA AMEFANANA NA MH FURANI... LAKINI BABA HALISI WA MTOTO BADO HAJAMUWEKA HADHARANI..!



Nakaaya 1
Kwenye picha za watoto na mama zao hii ni moja ya zilizonivutia! katoto kazuri sana.
Ni longtime kidogo ulikua hujamsikia Nakaaya na hii ni kwa sababu alikua na break ya uzazi akiwa ndio amejifungua mtoto wake wa kwanza nyumbani kwao Arusha.
Mwimbaji huyu ambae ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kutoa ile single ya ‘Mr. Politician’ sasa hivi anamiliki mawimbi na single yake mpya inaitwa ‘blessing’ aliyoifanya Noizmekah Arusha.
Nakaaya ameamua kuifanya hii single mpya kama dedication kwa mtoto huyu aitwae Kai kuonyesha ni jinsi gani amemgusa moyoni, vilevile kumpa ahadi ambayo ni mama pekee anaiweza.

BAADA YA DAVIDO KUNUNU GARI ZA KIFAHARI P SQUARE NAO WAJIBU MAPIGO ANGALIA HAPA KUFURU WALIYOIFANYA..!


magari mbili

Peter Okoye wa P Square ameonesha magari mapya ya kifahari yaliyoingia hivi karibuni katika garage ya familia yao.
Magari mojaAmepost katika Instagram picha kadhaa zinazoonesha magari hayo na kuandika maelezo yanayoonesha ni magari yaliyoingia katika jumba la Square Ville hivi karibuni na sio magari yote wanayomili.

“Crazy Squareville…New Arrivals…Don’t worry God will do same for u… #hardwork”
Magari mapya aliyoonesha ni pamoja na Wrangler Jeep ya mwaka 2014 ambayo kwa sasa inauzwa zaidi ya $22,395 na Bentley ya mwaka 2014 ambayo inauzwa kuanzia $177,500.
magari mbili



magari tatu

Friday, June 20, 2014

FILAMU YA SARAFINA YAENDELEA KUPIGWA MARUFUKU NCHINI MARUFUKU UKIKUTWA UNAONESHA SEHEMU ZA WATU UNAKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASKATA YAELEZWA INAWAKUMBUSHA WATU MACHUNGU YA UBAGUZI. XDEEJAYZ INAKUPALIVE







































Ile filamu maarufu Duniani ya SARAFINA iliyojinyakulia umaarufu mkubwa imeendelea kupigwa marufuku kuoneshwa sehemu za wazi na onyo kali limeendelea kutolewa na Serikali ya nchi hiyo kwa m2 yeyote atakaekutwa anaionesha filamu hiyo sehemu za wazi basi atakamatwa na kutupwa lupango bila huruma. Hata hivyo sababu ya kuizuina filamu ilielezwa ni jinsi ambavyo vizazi vipya havitakiwa kujuwa ukatili uliokuwa unafanyika miaka hiyo toka kwa Wazungu dhiti ya waafrika.
SOURCE: XDEEJAYZ TANZANIA

JINI LENYE MACHO 4 MBELE 2 NYUMA 2 LAONEKANA KWENYE SOKO LA MCHIKICHINI WAKATI SOKO HILO LIKIUNGUA DOKTA KAMDEGE ATHIBITISHA LILIKUWA NI JINI LA KUVUTIA BIASHARA..!



Kitu cha ajabu ambacho kinadhaiwa jini kilikuwa kimeonekana wakati soko likiungua huku kikiwa na macho manne nyuma mawili na mbele mawili huku yakiwa moto.
Hata hivyo kwa mujibu wa mganga maarufu wa wasanii na vingozi ambae ni mtaalam wa miti shamba Dokta Kamdege aliongea na blog hii kwa simu namba 0788-844490 alisema" Hiki kiumbe ni jini mali mara nyingi hutumika kuvutia wateja na mafanikio na hali madhara kwa binadamu bali ni rafiki mkubwa watu na lina mvuto wa kipekee ndiyo maana wafanyabishara wengi hulitumia kwa mafanikio ya biashara zao.

AIBU KUBWA MWANAFUNZI CBE DODOMA AVUNJA NDOA YA MTU AMPAGAWISHA MWANAUME HADI KUMUHONGA GAUNI LA MKEWE ALIVAA KWENYE UMISS BILA AIBU. XDEEJAYZ INAKUPA MKANDA MZIMA TEGA SIKIO..!


Chuo cha CBE DODOMA kimeendelea kutiwa najisi na baadhi ya wanafunzi wake wasio kuwa na maadili mema baada ya mwanafunzi mmoja wa kike mwenye picha yake huu kushoto akiwa na gauni la umiss kudaiwa kuisambaratisha ndoa ya mfanyabishara maarufu wa kisomari Mkoani Dodoma mwenye mkwanja wa maana na picha ya chini ni mke wa mfanyabishara huyo. blog hii kama kawaida kazi yake ni kuirekebisha jamii na kuipasha habari bado ina malizia vielelezo vya mwisho kabla ya kuanika ishu nzima hewani pamoja na picha kigogo huyo wa kisomari mwenye matukio mengi ya ukatili kwa wanawake.