TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, November 25, 2013

MAAJABU YA XTREME DEEJAYZ YAWASHANGAZA P SQUARE NDANI YA CLUB MAISHA, DVJ MAJEY NA ZUNGU MNYAMA WAWACHANGANYA WANAMUZIKI HAO WASEMA MAMBO HAYO HATA NIGERIA HAKUNA...!!!!



Na Sakina Sahabani
Katika hali isiyotarajiwa na wengi wanamuziki waliokuwa nchini mwishoni mwa juma na kufanya show ya aina yake na kuvunja rekodi ya show zote zilizowahi kufanyika nchini wanamuziki hao walionekan akufurahishwa na XTREME DEEJAYZ iliyokuw ikikamua kwenye kiota cha Burudani bongo Club Maisha huku wanamuziki hao wakiwemo.
Tukio lililotokea Ijumaa iliyopita wakati kundi hatari la utoaji burudani bongo la Xtreme Deejayz lilipokuwa mzigoni huku maelfu ya washuhudia, ambapo wanamuziki hao walifika ndani ya Club hiyo na kujionea vurugu za XTREME DEEJAYZ LIVE DRUMMER wakiwajibika ambapo wanamuziki hao walionekana kuchanganyikiwa na staili hiyo ya kimataifa huku wakisema kuwa kweli Tanzania iko juu kutokana na mambo hayo kwani hata nchini Nigeria kwao hamna labda Marekani na nchi nyingine za Ulaya.

XTREEM DEEJAYZ ilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wapatao elfu tatu na mia tano huku Zungu Mnyama kiwa na mzuka wa ajabu sambamba na Hyerpaman Hk. Hata hivyo kwa mujibu wa meneja burudani wa ukmbi huo Gila alisema Ijumaa hii kutakuwa hakutoshi kwani kundi hilo tena litafanya balaa kubwa.
GAZETI LA MASKANI BONGO HILOOO MTANI DESEMBA!

MAJANGA YAMKUTA SNURA, RADI LAMUUA KAKAAKE, LAMSAMBARATISHA VIBAYA SHINGONI, MASHABIKI WAMPA POLE!


  Na Sakina Shabani
Kaka wa mwanamuziki wa bongo flava na fimaku Snura Mushi ameuliwa na Radi la mvua na kumsambatisha vibaya.
 
Habari toma kwenye blog ya Hypermanhk ambayo iko chini ya meneja wake Hemed Kavu zilisema marehemu huyo aliyefahamika kwa jina la Yusuph Mushi alikuwa kwenye mihangaiko yake ya kutafuta ridhiki ndipo ajali hiyo ilipomkuta ambapo radi hilo lililokuwa kubwa lilimpiga na kumuharibu vibaya kisha kufariki papo hapo. 
Aidha Snura mwenyewe alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema msiba uko Mlandizi na wanatarajia kuzika leo
mashabi mbalimbali wa mwanamuziki huyo wanampa pole kwa majanga hayo huku wakimuomba Mungu ampe nguvu kwani kazi yake haina makosa
 MUNGU AMETOA NA SASA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!
 
MASKANI BONGO. MASKANI BONGO, MASKANI BONGO JITAYARISHE KUPATA KOPI YAKO MAPEMA MWEZI UJAO!

Sunday, November 24, 2013

HII NDIYO TAARIFA YA ZITTO KABWE LEO KWA VYOMBO VYA HABARI. MARA BAADA YA KUPOKWA MADARAKA YOTE MAKUBWA NDANI YA CHADEMA!



1. Utangulizi Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. 

Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013.   Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu . Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. 

Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.
  Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika. 
Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA.  Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho. 
  2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu.
 Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. 
Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama. 
  i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

  • Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.
  • Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.
  • Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.
  • Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.

ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua. 
  iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini.
 Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. 
Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho. 
  iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea.
 Mwaka 2012 baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko. 
  v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae. 
Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo:

  • Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilisha
  • Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.
vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

  • Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.
  • Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.
  • Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.

3. Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA.  Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:

  1. Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.
  2. Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.

4. Hitimisho Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania.
 Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'.
 Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. 
Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.
  Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.
  Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.
 
Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. 
  Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. 
Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.
  Kabwe Zuberi Zitto, Mb Dar es Salaam. 24 Novemba, 2013 

"GAZETI LA MASKANI BONGO LITAKUJIA HIVI KARIBUNI KAA TAYARI KUPATA KOPY YAKO KWA TSH 500 TU!"

MALAWI KUNA KITU INAKITAKA TOKA TANZANIA, RAIS WAKE ATANGAZA MKOA WA RUVUMA NA WANANCHI WAKE NI MALI YAKE ...!!



RAIS wa Malawi, Joyce Banda ametajwa kuendeleza chokochoko baina ya nchi yake na Tanzania, huku sasa akidaiwa kutumia redio na runinga za nchini mwake kutangaza kuwa mkoa wa Ruvuma, viongozi na wananchi wa ukanda wa Ziwa Nyasa ni mali yake.
Aidha, amesitisha safari za meli ya mv Ilala iliyokuwa ikifanya safari kwenye Ziwa Nyasa kusafirisha mazao na wananchi wa ukanda huo upande wa Tanzania.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa soka wa Mbambabay jana, Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba, alisema Rais Banda ambaye aliibua upya mzozo wa mpaka baina ya nchi hizi mbili, kuwa ni mkorofi kutokana na kufanya vitendo vinavyoonesha uhusiano baina ya nchi hizi mbili kuzorota.
Komba alibainisha vitendo hivyo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema imefika mahali Rais Banda anapotosha ukweli kuhusu mpaka kati ya nchi hizo mbili na kudai sehemu ya mwambao wa Ziwa upande wa Tanzania ni yake.
Mbunge huyo alisema jimbo la Mbinga Magharibi ambalo ni Wilaya ya Nyasa, wanasikiliza matangazo ya redio za Malawi, na anazitumia kupotosha umma kuwa ukanda wa Ziwa Nyasa ni mali yake na wananchi wanaamini hivyo.
Rais Banda anatangaza kupitia vyombo vya habari vya nchi yake ambavyo vinasikika vizuri katika wilaya hiyo kutokana na wilaya ya Nyasa kutopata mawasiliano ya redio na runinga za nchini. Komba alisema kutokana na wilaya hiyo kukosa mawasiliano ya vyombo vya habari, wananchi wake wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba za viongozi wa Taifa.
Wananchi wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba ya Rais Kikwete ya kila mwezi na hotuba za viongozi wengine wa kitaifa wakiwamo Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Kutokana na kukosekana usikivu huo, Rais Banda anatumia nafasi hiyo kutangaza kuwa viongozi wote wa wilaya na mkoa na eneo lote ni mali yake,” alisisitiza Komba. Aliongeza kwamba watu wote walioko kwenye mkutano huo isipokuwa Katibu Mkuu Kinana, akiwamo Dk Asha-Rose Migiro ambaye alizaliwa Mbambabay wote ni mali ya Rais Banda.
Mbunge huyo alisema wananchi wa eneo hili nao ni Watanzania wanaostahili kusikia na kupata habari za nchi yao, badala ya kusikiliza nyimbo na matangazo ya Malawi ambayo yanakuwa na ajenda zake.
Mbunge Komba alimwomba Katibu Mkuu Kinana kwenda kuhimiza kutekelezwa haraka kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuleta meli ili kuwa na usafiri wa uhakika wa mali na wananchi katika eneo hilo.
Kinana alisema ahadi ya meli ya Rais, hiyo ana uhakika itatekelezwa na kufafanua kuwa meli tatu zinatengenezwa Korea Kusini na zitakapokamilika ya Ziwa Nyasa itapelekwa kutoa huduma.
Alisema baada ya Banda kuondoa meli hiyo wananchi wa Mbambabay wanatumia boti dogo kusafirisha abiria na mizigo, hali ambayo inatia shaka.
Kinana alisema amesikia kilio cha Mbunge Komba, kwamba ahadi ya Kikwete itatekelezwa ili kuwapa wananchi usafiri wa meli, ingawa itatumia muda kutokana na kuhitaji muda mwingi kubuni na kutengeneza.
"JIANDAE KUSOMA GAZETI PENDWA JIPYA LA MASKANI BONGO HIVI KARIBUNI LITAKUWA MTAANI"

HUYU NDIYE DIREKTA ALIYETUMULIWA NA WEMA SEPETU KWA KUIGEUZA GARI YAKE GUEST!


Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa mwanadada Wema Sepetu ameamua kumtimua  aliyekuwa director wake maarufu kwa jina la Chid ni ufuska uliokubuhu wa director huyo ambaye alikuwa akitumia magari ya Wema Sepetu kama gest ya kumaliza haja zake. 

Wema aliamua kuchukua maamuzi hayo magumu ili kunusuru kashfa kubwa ambayo ingeweza kuikumba kampuni yake.

Kwa mujibu wa tovuti ya bongoclantz ya kupata taarifa hizo Wema aliamua kumtimua Chid kwenye kampuni yake ili kulinda heshima ya kampuni hiyo ambapo Chid na vijana wengine walikuwa wakitumia gari hiyo kung'olea watoto wakali na kuwachapa ndani ya gari hiyo. 
"Hii ilitokana na upendo wa mashabiki kwa Wema na wasichana wengi walikuwa wakiiona ile gari wanaingia wenyewe kwenye gari wakidhani ndani yuko Wema, hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Chid na wenzake kuwamaliza wasichana hao

GAZETI LA MASKANI BONGO LITAKUWA MTAANI HIVI KARIBUNI KAA TAYARI NI GAZETI PENDWA NAMBA 1 TANZANIA USIKOSE!

TIZAMA SHOW YA P SQUARE LIVE KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB EAST AFRIKA TV, REDIO WADHIHILISHA UBABE WA KUTISHA KWENYE UANDAAJI WA MATAMSHA WANANCHI WASIFU ULINZI MKALI!


Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square wakilivamia jukwaa la Leaders usiku huu.…
Joh Makini akilitawala jukwaa.
Nikki wa Pili (kushoto) na G Nako wakifanya yao…

LADY JAYDEE AKIFANYA YAKE STEJINI

Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee' au 'Anaconda' akiwapagawisha mashabiki wake waliohudhuria katika Viwanja vya Leaders Club usiku huu katika shoo wa wakali P-Square.…
MC Dullah akiwa kazini.

BEN POL AKILISHAMBULIA JUKWAA KATIKA YA SHOO YA P-SQUARE

Mwanamuziki Ben Pol akiwasha moto katika steji ndani ya Viwanja vya Leaders usiku huu katika shoo ya P-Square Live in Dar.…


Saturday, November 23, 2013

LULU AWAKERA WASOMAJI WA MITANDAO WAMSHUSHIA MATUSI MAKUBWA, SIFA ZAMPONZA!!!



Mashabiki hao wamemtolea uvivu lulu baada ya kusema kuwa hawezi kumvulia nguo Diamond hali iyozusha mjadala na matusi juu toka wasomaji wa mitndao.

HIZI NDIO KOMENT ZA WASOMAJI, HUKU AKISHAURIWA KUWA MAKINI NA KAURI KWANI KAMA HANA KITU CHA KUSEMA NI HERI AKAKAA KIMYA KULIKO KUROPOKA!!
 
GAZETI JIPYA LA MASKANI BONGO LITAKUWA MTAANI HIVI KARIBUNI KAA MKAO WA KULA KUPATA HABARI TOFAUTI ZA MASTAA WA NDANI NA NJE YA NCHI KWA SHILINGI MIA TANO TU!