TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, September 27, 2013

MSANII HUYU WA BONGO MOVIE KUNA SIKU WATAKUJA KUMBAKA HADHARANI KWA MAVAZI YAKE YA NUSU UCHI, APEWA ANGALIZO!!!

 
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa kutokana na kukatiza kitaa akiwa na nguo iliyombana na kuonesha makalio yake yaliyojazia.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, tukio hilo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita maeneo ya Mwenge, jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa ameenda kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali ndipo kundi la wanaume wakware lilipoanza kumzomea.

Tukio hilo lilimfanya Amanda apoteze amani ghafla na kuamua kutimka zake eneo hilo huku akiwashangaa. Paparazi wetu hakuwa nyuma, alimpigia simu na kumuuliza kulikoni?
“Daah! Ilikuwa kero kweli, wanaume wazima wanaacha kazi zao na kuanza kunizomea huku wakiniambia kuwa ni dawa za Kichina. Lakini ukweli ni kuwa hii ni asili yangu na si Mchina,” alisema Amanda.
Hata hivyo msanii huyo amepewa angalizo na wadau kuwa kuna siku atakuja kufanywa kitu mbaya na wahuni kutokana na uvaaji wake wa nusu uchi awe mwangalifu sana.

WIKI MBAYA KWA AJALI TANZANIA, INASIKITISHA JAMANI!

Mwili wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashidi Seleman mkazi wa Isevya manispaa ya Tabora ambaye amepoteza maisha baada ya Lori walilokuwa wamepanda kuanguka eneo la Inala barabara ya kwenda Kigwa,Polisi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye amekimbia huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa vibaya ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Tatizo la ukosefu la ukosefu wa vifaa vya kuokolea vilisababisha maiti ya mtu huyo kukaa muda mrefu akiwa amebanwa na Lori hilo ambalo ni mali ya kampuni ya mkandarasi JOSSAM


Awali jitihada za Polisi na wananchi ziligonga mwamba na kubaki wakiiangalia maiti hiyo pasipo msaada wowote ajali ambayo imetokea majira ya saa kumi jioni hapo jana.

Askari wa usalama barabarani wakiongozwa na kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Swaleh Digega hatimaye wakafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo na kuupeleka hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kuuhifadhi....Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX

Thursday, September 26, 2013

SIRI IMEFICHUKA KUMBE DEREVA BODABODA ALIYEGONGWA NA GARI AKUNYWA VIROBA KABLA YA KUENDESHA PIKIPIKI HIYO!

 

Ajali mbaya iliyotokea  barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini musoma kuelekea kamnyonge.  
Kamera yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.

Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.
Aidha taarifa zilipatikana baadae zilizema dereve bodaboda huyo baada kufikishwa hospitali alionekana akinuka pombe hali iliyoonesha kuwa alilewa kabla ya kuendesha pikipiki yake.

 
 
 
 
 
 
 

AL- SHABAAB WALIPUA KITUO CHA POLISI NCHINI KENYA LEO HII, POLISI WAWILI WASAMBARATISHWA VIBAYA NA MAROKETI YA KUTUNGULIA VIFARU!





Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa watu wanaozaniwa kuwa ni magaidi wamevamia kituo cha Polisi katika Mji wa Mandera nchini Kenya na kuwaua polisi wawili, watatu wamejeruhiwa vibaya na baadaye kuchoma magari zaid ya 11

MREMBO ANUSA MAUTI BAADA YA KUPASULIWA TAYA NA MUMEWE BAADA YA KUMFUMANIA NA RAFIKI YAKE WA KARIBU!


Hapa akiwa amelala hajitambui baada ya kupata kipigo


Hapa wananchi wakiwa wanashudia jamaa akimpa kichapo mkewe baada ya kumfumania

Picha hii jamaa amembeba mke wake baada ya kumfumania na kumpa kipigo kikali wakielekea nyumbani
Tukio hili limetokea leo asubuhi mida ya saa 8.00,katika mji wa Iringa maeneo ya mwangata paparazzi wetu alifanikiwa kulinasa hili tukio.Jamaa mmoja jina halikuweza kupatikana amemfumania mkewe gesti baada ya kumfumania alichokifanya ni kumruhusu yule mwanaume aliyemfuma na mke wake nakusema jamaa hana kosa mwenye kosa ni mke wake.Jamaa akazidi kufunguka nakusema mke wake alitakiwa kukataa alipotongozwa moja kwa moja mke wangu ndiye mwenye makosa huyu mgoni hana kosa kabisa.Kilichofuata baada ya hapo alimpa kichapo kikali kama unavyoona kwenye picha. Mwisho wa siku akambeba na kurudi naye nyumbani maeneo ya mwembetogwa ili kumfungashia mizigo yake na kumrudisha kwa wazazi wake.

SIWEZI KUPIMA UKIMWI HATA KWA MTUTU WA BUNDUKI AU NIFUNGWE MINYORORO SITHUBUTU NG'OO!



STAA wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa hana mpango wa kupima ‘ngoma’ kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
Akiongea na paparazi wetu, Johari alisema hakufurahishwa sana na taarifa hizo za kupima ugonjwa huo na kusema ukweli ni kwamba yeye hajawahi na wala hana mpango wa kupima hata akifungwa minyororo.
Nachukia sana watu kusema kuwa eti tunapimisha watu Ukimwi, nahisi kuna mtu anataka kunichafulia tu. Sisi wote hapa RJ hatujapima Ukimwi wala hatuna mpango wa kufanya hivyo,” alisema Johari.

WIKIENDI YA HISIA ZA BURUDANI NDANI YA NEW CLUB MAISHA DAR 001. NEW CLUB MAISHA DODOMA 002 . NEW CLUB MAISHA MTWARA 003. NEW CLUB MAISHA MBEYA 004. HAIJAWAHI TOKEA NI MZUKA ZAIDI YA MZUKA!