TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, July 22, 2013

SINTAH AJIBU MAPIGO KWA SHILOLE, AMWAMBIA ANAKISUBIRI KWA HAMU KICHAPO CHAKE, MASHABIKI WAMUUNGA MKONO SINTAH!

 Msanii nyota kitambo kwenye game ya ugizaji Sintah.
 Sintah.
Msanii wa muziki na maigizo nchini Shilole ambae ametangaza kumvulumushia makonde mazito Sintah popote atakapomuona.
Na Livingstone Mkoi
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya afrika na kati Sintah amefunguka kuhusu vitisho anavyopewa na msanii mwenzake wa muziki na maigizo Shilole kuwa ajiandae kuchezea kipigo cha mbwa mwizi popote atakapomuona.

Akiongea kwa njia ya simu toka nyumbani kwake Sintah baada ya mtandao huu kutaka kueleza anachukuliaje vitosho hivyo vya Shilole ambapo alisema" Kaka naambiwa sana na watu hasa wanaofatilia mitandao eti natafutwa kupigwa na Shilole sasa ninacho shangaa huyo Shilole anapafahamu kwangu aje basi anipige au kwenye ofisi zangu anapajua namkaribisha vizuri sana jamani" Alisema Sintah

Aidha Sintah aliongeza kusema kuwa" Mimi huwa sio mtu wa maneno yeye aje tu anipige na sio kutangaza kwenye mitandao kuwa ananitafuta anipige hayo mambo ya bifu siku hizi watu wanayachukulia upuuzi kutafuta pesa ndio mpango mzima hivyo mimi namshauri Shilole kama underground wa sanaa nchini aachane na bifu badala yake akazane kwenye mambo yake ya kutafuta pesa kwa ajili ya maisha yake na familia kwani uzee unakuja" Alisema Sintah

Sunday, July 21, 2013

MSANII BONGO MOVIE AJIRUSHA JUU GHOROFA YA 5,AVUNJIKA MIGUU YOTE NA KIUNO


  Hapa kama inavyoonekanamiguu ya  Gado Balotel  na bandeji baada ya kuvunjika yote mara baada ya kujirusha toka ghorofa ya 5



  Mshare unamuonesha  Gado Balotel  akiwa kwenye kava la moja ya filamu zake alizocheka kabla ya kukumbwa na balaa hilo.
 Msanii na Kiongozi wa kundi la Bongo Muvi nchini JB ambae ameombwa na wasanii kuchangisha harambee haraka ili kupata fedha za kumsadia msanii mwenzao huyo anaeishi kwa mateso makali.
  Msanii na mwanamasumbwi wa zamani Fike Wilson ambae amepongezwa na wadau baada ya kujitolea kumsaidia msanii huyo, ambapo kwa sasa anaishi nyumbani kwa Fike huku akiwa anabebwa kupelekwa chooni na kurudishwa pia.
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Saimon Mwakifwamba nae pia ameombwa kuungana kwa pamoja na wasanii wengine kumsaidia msanii mwenzao anaishi kwa mateso makubwa usiku na mchana.

Na Livingstone Mkoi

Msanii nyota toka kiwanda cha muvi za kibongo nchini Maulidi Mfaume maarufu kwa jina la Gado Balotel sasa amekumbwa na balaa la aina yake baada ya kuvunjika miguu yote miwili pamoja na nyonga kuteguka baada ya kudondoka toka ghorofa ya nne alipokuwa akiigiza filamu ya msanii mwingine aitwae Baga.

 

Baada Xdeejayz na kituo cha luninga cha DTV kupata taarifa hizo lilipiga hatua ndefu hadi mahala anapojiuguzia msanii huyo ambako ni nyumbani kwa msanii Wilson Fike maeneo ya Home Alone Vijana Kinondoni na kuonana uso kwa uso na msanii huyo aneishi kwenye maumivu makali.

 

Akiongea na mwandishi wetu nyumbani hapo Balotel alisema alikutwa na balaa hiyo wiki mbili zilizopita akiwa Location ndani ya hotel ya Con Way iliyopo Magomen Kagerana wasanii wenzake kama Hemed, Baga, Manaiki Sanga na wengineo wakati wakiigiza.

 

Balotel aliendelea kusema kuwa wakati shughuri za kuigiza ziliendelea na kuna sini moja iliyokuwa inahitajika kuigizwa kwa mfano ikimtaka mtu aigize kama anataka kujirusha kwenye ghorofa lakini asiruke ili kameraman  kuchukua picha achukue shoti hiyo kisha mtu huyo aende chini kisha achukuliwe shoti nyingine ya kujifanya ametua chini.

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa nafasi hiyo ilibidi aigize msanii mwenye filamu Baga lakini kutokana na uwoga wa msanii huyo alikuwa akijishauri namna ya kuigiza kuruka ghorofani ndipo Ballotel akamtoa pembeni na kumuonesha namna ya kuruka kama Jet Lee huku akimwambie mwenzake hiyo ilikuwa kazi ndogo sana.

 

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa baada ya hapo alijikuta ameruka toka ghorofa ya nne, lakini aliendelea kusema“ Wakati nikiwa bado sijashuka chini njiani nilianza kuhisi harufu ya kifo kwani tayari nimuona Israel mtoa roho akinipungia mkono na hatimae nilitua chini  kwa kufikia miguu” Alisema  Ballotel

 

Hata hivyo kijana huyo aliongeza kusema kuwa mala baada ya kutua nchini alihisi moto unawake miguuni mwake huku harufu ya damu ikimtoka puani na mdomoni na baada ya kujiangalia aliona visigino vyake vikiwa vimepasuka vyote huku tumboni kukiwa na maumivu makali sana kumbe wakati huo nyonga ilikuwa imeachia huku miguu yake ikiwa imesogea tumboni.

 

Gado alisema baada ya tukio hilo wasanii wenzake walimchukua na kukmimbiza Hospital ya Mwananyamala mbapo dakika chache baadae walimkimbiza Muhimbili kwa matibabu zaidi.Msanii huyo ambae ametamba sana kwenye filamu kama Going Bongo,Msitu wa Hifadhi,Tumbo Joto na Escap ambayo alikuwa akiigiza siku ya tukio lililomkuta.

Aidha msanii huyo aliendelea kusema kwa sasa anaishi kwenye mateso makali huku wasanii wenzake wakishindwa kumpa ushirikiana “Hapa nilipo nalelewa na Fike Wilsoni ndiye anaenibeba kwenda chooni na kunirudisha kwa kweli hali yangu sio nzuri nahitaji msaada wa wasanii wenzengu, Wako wanaokuja kunirushia chochote kama

 

Kalapina,Young Killer na madaktari wanasema huenda wakanishauri kwenda India ili wakazirekebishe nyonga zangu” Alisema Gado na kuongeza kuwa anawaomba wasanii wenzake wasamalia wema kumsaidia kwani hali yake ni mbaya na huenda kwa mujibu wa madakatari wake akahitajika kupelekwa India ili kukinusuru kiuno chake la sivyo hatozaa tena kwa vile nyonga vimeshafyatuka.

Saturday, July 20, 2013

UNYAMA WA KUTISHA SERIKALI YA KONGO KUSHITAKIWA KWA KUDHALILISHA MAITI ZA WAASI WA M23!

 


 Goma -DRC.


 

WAKATI mapigano yakizidi kuwa makali kati ya wanajeshi wa DR Congo (FARDC) na kundi la waasi wa M23, wanajeshi wa DRC wako hatarani kushitakiwa kwa tuhuma za kuwatesa waasi na kunajisi maiti zao.




 

Friday, July 19, 2013

MASHEKH WAMLANI VIKALI WEMA SEPETU KWA KUANIKA MATITI YAKE MTANDAONI NA NDANI YA MWEZI MTUKUFU! 

 
“Did I miss a spot…? I dunno,” ni maneno ya Wema kwenye picha aliyoiweka leo katika mtandao wa Instagram. 


Hata hivyo mashabiki wengi wamemshambulia mrembo huyo kwa kile wanachohisi hakupaswa kuiweka katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. 

UCHAWI WAIBUKA TAZARA: NJIWA ATUA NA BARUA YA VITISHO OFISINI WAFANYAKZI,BOSI WAO WATIMUA MBIO NA KUACHA OFISI!


 


Njiwa akiwa na ujumbe wa barua kama inavyo onekana

SERIKALI YASISITIZA KUWA "KODI YA LINE ZA SIMU" IKO PALE PALE HAKUNA MJADALA!

 


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

AIBU NZITO, MISS UTALII TANZANIA APIGA PICHA ZA UCHI,HALAFU NI MTOTO WA SHEKH MKUBWA TU NCHINI

 Mshiriki Miss Utalii Taifa 2013 Fathiya Masoud maarufa kwa jina la Mrembo wa Facebook.
 Mrembo wa Facebook.
Hapa Mrembo wa Facebook akiwa ameanza kuvua nguo taratibu ilikuwa kama masihala vile.


 

  Fathiya hapa ameamua kuvua kabisa ili kubaki na chupi peke yake.