TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, March 29, 2013

PICHA ZA JENGO LILILOANGUKA LEO KARIAKOO


Kwa maelezo ya shuhuda, inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.
Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti nne.
Sehemu ya chini zinaonekana bado nzima hazijadondoka ila kifusi cha kutoka juu ndio kimefunika lakini kuna watu ndani yake wako hai na inaripotiwa wanapata hewa vizuri na wamekua wakiwapigia ndugu zao na kuwaita waje kwenye eneo la tukio.

XTREME PICTURE OF THE DAY


KIWANJA KIPYA CHA BURUDANI KIMEFUNGULIWA KINONDONI THE JACARANDA

 

 THEJACARANDA ndio jina la chimbo jipya la vijana lililopo maeneo ya kinondoni pembeni ya bar ya UHURU PICK na inatizamana na MANGO GARDEN. Tukiongea na manager wa kiwanja hiko cha kijanja JULIE alisema '' jumamosi hii ya mkesha wa pasaka ndio kitazinduliwa rasmi kabisa ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali,na muziki mnene utakaoporomoshwa na madeejayz wakali wa hapa jijini,

 Kiukweli ni sehemu nzuri sana ambayo unaweza ukakaa na kufurahia,na kujisikia ukiwa comfortable kabisa

 Patakuwa panafunguliwa kila siku kuanzia jumatatu mpaka jumapili,utapata vinywaji baridi na chakula cha moto kabisa.

 NI Sehemu ambayo inaweza kuwakutanisha watu tofauti ,wakiwepo wale wastarabu,na madili yao wanaweza kukutana hapo muda wa mchana nakuongea bila bugza yoyote ile.

 Huyu ndio mANager wa hii club ya jacaranda

 Mandhari tulivu kabisa

 Kutakuwa kunapatikana SHISHA,kuna sehemu ya SMOKING ROOM,NA vyoo vyakutosha kwa kila jinsia.

 Kwa wale wapenda SOKA kuna big screen kila kona ya club hii, na wanaonyesha  mpira kutoka kwenye LIGI za ukweli dunia muda wowote.











Kutakuwa na kiiingilio siku za wikiend hili kupata burudani safi kabisa