TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, January 28, 2013

MASIKINI MSANII MATUMAINI AFYA YAKE NI MBAYA,WATANZANIA WATAKIWA KUMUOMBEA!

Msanii nyota wa komedi nchini Matumaini ambae inadaiwa anaumwa sana na hali yake ni mbaya huko nchini Msumbiji ambako alikuwa anaishi huko.

NISHA ADAKA UJAUZITO,DALILI ZOTE WAZI!


YADAIWA EMEJAZA EMBE MBICHI,MBILIMBI
 KWENYE FRIJI YAKE!
Aongea na Xdeejayz na kuweka wazi kila kitu.

Na Livingstone Mkoi
Msanii nyota kwenye kiwanda cha filamu za kibongo Salma Jabu " Nisha" Anahisiwa kuwa ana ujauzito tena unaokadiliwa kufikia miezi miwili na siku kadhaa.
Habari za uhakika zilizoifikia Xdeejayz toka kwa mashosti wa msanii huyo zilisema kuwa" Haki ya Mungu Nisha amenasa ujauzito kwani anadalili zote za ujauzito nyumbani kwake friji imejaa maembe mabichi,mbilimbili pamoja vifuko vya udongo" Alisema msichana huyo ambae ni rafiki mkubwa wa Nisha.

Aidha dalili nyingine msanii huyo amekuwa anatema tema mate ovyo huku akilalamika kusikia kizunguzungu"Jamani mimi ni mwanamke najuwa A-Z ya dalili za ujauzito Nisha amenasa hata ukimuangalia usoni utajuwa tu pia amekuwa akipenda samaki wa kukaanga na ndimu nyingi ndio chakula chake" Kilisema chanzo cheti 
Hata hivyo xdeejayz ilinyanyua mkonga wa simu na kumcheki hewani Nisha ili kuthibitisha madai hayo ambapo alipatikana na kusema kila kitu" Jamani mimi sio kwamba nini mimba isipokuwa nimeridhika tu na maisha ndio maana naiva na sio ujauzito, na pia napenda sana kula vitu vya ugwadu gwadu kwa ajili ya mapenzi binafisi" Alisema Nisha.


Thursday, January 24, 2013

HALI YA BABA WA 20% PACENT SIO NZURI ALAZWA MUHIMBILI!

Mwanamuziki 20% Pacent 
Na Livingstone Mkoi
Baba mzazi wa mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Abasi Kizansa (20% Pacent) mzee Kizansa inadaiwa hali yake sio nzuri kutokana na upasuaji aliofanyia hivi karibuni.

Akiongea na xdeejayz kwa sharti la kutotajwa jina lake mmoja wa wadogo wa mwanamuziki huyo alisema kuwa baba yao hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa tumbo kwa maradhi ambayo hakuyataja.
Hata hivyo hadi jana Jumatano usiku kulikuwa na taarifa kuwa mzee huyo anaeishi Kimanzi alizidiwa na kurudishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Xdeejayz ilimtafuta mwanamuziki huyo kupitia simu yake ya kiganjani  ili kuzungumzia zaidi taarifa hizo lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana.

Wednesday, January 23, 2013

MACHANGUDOA WA KITANZANIA WAVAMIA AFRIKA KUSINI KUWANASA NYOTA WA SOKA!

 Mwanadada aliyefahamika kwa jina moja la Ashura ambae ni mtanzania toka Mkoa wa Tanga akiwa kwenye viunga vya mji wa Durban nchini Afrika Kusini.Ambako ametua kwa ajili ya kuwanasa wachezaji wa mpira kwenye mashindano ya kombe la Afrika yanayoendelea nchini humo. 

 Hapa ni machangudoa wakiwa mitaani usiku kuwasubiri wanaume pamoja na wachezaji wanaohitaji huduma ya mapenzi.

Na Mwandishi Wetu aliyeko Afrika Kusini

Katika hali isiyokuwa ya kawaida changudoa mmoja ambae ni mtanzania aliyefahamika kwa jina la Ashura ambae ni mzaliwa wa Mkoa wa Tanga amevamia nchini Afrika kusini kwenye mashindano yanayoendelea kwa lengo la kutoa burudani kwa wanasoka wanaoendelea na michuano ya soka nchini humo.

Habari za uhakika zilizoifikia xdeejayz ambazo hazina hata chembe ya uwongo zinasema kuwa dada huyo changudoa ni kibogo kwa mastaa wa kiume kwani ana mbinu nyingi za kuwanasa hasa kutokana na uzoefu wa siku nyingi aliokuwa nao kwenye kazi yake hiyo.


Wednesday, January 16, 2013

SNURA KUITEKA DAR LIVE JANUARI 26!

Mwanamuziki Snura Mushi akifanya vitu vyake.

Wacheza shoo wa Snura wakikamua jukwaani, ambapo wacheza shoo hao wameapa kuvitegua viuno vyao jukwaani siku ya June 26 ndani ya Dar Live Mbagala kwenye shoo iliyoandaliwa na shirikisho la filamu Tanzania TAFF kwa ajili ya kuchangia ofisi ya Bongo Muvi pamoja na Comedian.





Video mpya ya Snura "Debe la Vanga"


Na Livingstone Mkoi

Mwanamuziki anayechipukia akitokea kwenye filmu Snura Mushi Januari 26 mwaka huu anatarajia kuwathibitishia mashabiki kuwa yeye ni moto wa kuotea mbali kwenye muziki atakaposhusha bonge la shoo kwenye uwanja wa taifa wa burudani Dar Live.

Akipiga stori na Xdeejayz meneja wa msanii huyo Hemed Kavu alisema kuwa msanii wake alikuwa kambini toka tarehe tano mwezi akifanya mazoezi na kundi lake kwa ajili ya video ya wimbo wake mpya aliouita jina la "Debe la Vanga" ambapo kwa sasa video yake iko ndani tv mbalimbali.


Aidha HK aliongeza kusema kuwa "Mikakati ya Snura mwaka huu ni kufikia kilele cha mafanikio kupitia muziki na kuanzia shoo hii ya tarehe 26 atafanya maajabu makubwa kwa staili yake mpya ya uchezaji ambayo tunaamini mashabiki watachanganyiwa watakapoiona" Alisema Hk


Hata hivyo nae Snura aliieleza Xdeejayz kuwa mwaka huu hataki mchezo kabisa kwenye mambo yake ya kazi kwani mwaka uliopita alitumia kujitambulisha kwa mashabiki wake na anashukuru walimpokea vyema. Lakini mwaka huu ni kazi tu hadi kieleweke.

Bonge la Shit kutoka kwa Baby Elice sikiliza

Sikiliza ngoma ya Baby elice je unajua mlegezo kazungumzia nini?
New Track Kutoka T.M Power anajulikana kama Baby Alice ..Akiwa Collab na Muki wa Makomando ..Mpango umesimamiwa na c9. kIRI rECords. Contact : +255652171025 Email : D120dw@gmail.com

KAMANDA KOVA AWAWEKA KITI MOTO CHARLES KENYELA NA ENGELBERT KIONDO KUHUSU MACHANGUDOA!

 Kamanda wa polisi Kanda ya Dar es Salaam Bwana Suleiman Kova.
Kamanda wa polis kanda ya Kinondoni Charles Kenyela.

Kikao chachukuwa siku nzima kuweka sawa tofauti zao.

Na Mwandishi Wetu
Kamanda wa polisi kanda maalum Jijini Dar es Salaam Bw Suleiman Kova kushirikiana na maofisa wa ngazi ya juu toka makao makuu ya polisi wamewaweka kiti moto makamanda wa mikoa ya kiposi Temeke kamanda Engelbert Kiondo RPC Temeke na Charles Kenyela RPC Kinondoni kufuatia kutofautiana kuhusiana ishu ya makahaba.
Habari za uhakika zilizonaswa na Xdeejayz kushirikiana chanzo chetu toka polisi central zilisema Kamanda kova alifikia uamuzi wa kufanya kikao hicho cha haraka mapema wiki kwa kuwaita makamanda hao kufika ofisini kwake ili kuzungumzia sakata hilo.
Habari zaidi juu ya kutofautia kwa makanda hao zilisambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari mapema wiki zikimnukuu kamanda wa polisi Temeke kumshutumu kamanda wa polisi Kinondoni kuwa hajui sheria kwa kuendelesha uparesheni ya kuwakamata machangudoa na kuwapeleka mahakamani wakati hakuna sheria inataka wanawake hao wafikishwe mahakamani kwa tuhuma hizo badala yake Kenyela alitakiwa kuwapa elimu kuacha kufanya hivyo kwani kuna athari nyingi ambazo zinaweza kuwakuta.
Kufuta kauli hiyo Kamanda Kenyela nayeye kupitia vyombo vya habari alieleza kusikitishwa sana na kauli ya kamanda Kiondo kuingilia utendaji wake wa kazi na kusema kuwa amedhalilishwa sana na isitoshe yeye ana simamia mkoa mwingine na labda kama angeona kuna sehemu kuna mapungufu basi angempigis simu na kumueleza kuliko kuzungumzia ishu hiyo kwenye vya habari.
Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo chetu haikufahamika hitimisho la kikao hicho kwa utofauti huo.