TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, December 13, 2012

NJEMBA LAOLEWA HARUSI YA KIFAHARI NA MUME WA MTU!

Mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Brick akiwa mwenye furaha baada ya kufunga ndoa ya kifahari na bwanaake ambae anadaiwa ni mume wa mtu.
Na Mwandishi Wetu
2012 unaisha na vituko vya kukumbukwa kufuatia matukio ya kihistoria kuandikwa.
Mwanaume mmoja nchini India katika mji wa Ujjain Ancient aliyefahamika kwa jina la Brick ameolewa ndoa ya kifahari na mume wa mtu.

Habari za uhakika toka kwenye mtandao mmoja nchini humo unaosifika zaidi kuandika habari za uchunguzi ulisema kuwaa Brick mwenye umbo lililojengeka vizuri amekuwa akijihusishwa na vitendo vya ngono ya jinsia mojaa na mumu huyo wa mtu hadi kupelekea kuoana kabisa.
Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa ndoa hiyo liyofungwa nje ya mji anaoishi kijana huyo na ilifana sana kutokana na sherehe kubwa na ya gharama kufanyika ambapo watu walikula na kusaza huku dume hilo lililoolewa likiwa lenye furaha tele huku likiahidi kuwa sikivu na kumpa mapenzi moto moto mumewe huyo ambae kwa mujibu wa mtandao amemzidi miaka mitani Brick.

RICK ROSSE WA BONGO ANUSURIKA KIFO KWA AJALI MBAYA,AVUNJIKA MBAVU MBILI!

 David Shahid Rick Rosse wa Bongo.

  Rick Rosse wa Bongo.
Na Livingstone Mkoi
Kijana wa kitanzania David Shahid ambae miezi ya hivi karibuni alitokea kujizolea umaarufu kutokana na kufanana sana sura na mwanamuziki toka Marekani Rick Rosse hivi karibuni amenusurika kupoteza maisha baada ya kupata ajali mbaya ya gari alipokuwa kazini.

Rick Rosse amesema kuwa alipata ajali hiyo alipokuwa kwenye mizunguko yake kazini maeneo ya Kurasini Jijini Dar ambapo hadi sasa ni wiki ya tatu yupo hoi kitandani kwani amevunjika mbavu mbili na kujeruhiwa vibaya mgongoni.

Wednesday, December 12, 2012

SWAGA ZA JB MKUU WA MAJAJI ZAWAPAGAWISHA MASHABIKI JANGWANI KWENYE SHOO YA NI WAKATI WAKO TOUR 2012 NA DTV

 MWANAMUZIKI JB MKUU WA MAJAJI AKIWA STEJINI KUWAPA
 RAHA MASHABIKI WAKE!

MWANAMUZIKI JB MKUU WA MAJAJI AKIWA STEJINI KUWAPA
 RAHA MASHABIKI WAKE!
Msanii nyota kwenye muziki wa bongo flava 
JB MKUU WA MAJAJI amekuwa na swaga flani zinazowachengua mashabiki kila kukicha kiasi cha kukosa raha pindi asipoonekana kwa steji.
Tukio la kukosa muda wa kusema maneno yake kwenye tamasha la tarehe 9 mwezi huu katika viwanja vya Jangwani yalionekana kuwakera mshabiki hao.
JB anasifika sana kwa kuongea maneno ya kihuni ambayo mara nyingi huwafurahisha mashabiki wake ambapo moja ya maneno ambayo mkuu huyo wa majaji hupenda kuyasema ni " Wali Funza Mchuzi Mende, Usinipe buku nipe mia saba sabini.Anaekula kuku na mimi kaputu time ikifika wote tutakwenda chini kudadeki" Mananoi hayo huwakuna sana mashabiki kiasi cha kupagawa.
JB ni mmoja wa wasanii waliwahi kutamba sana miaka ya nyuma wakiwa kwenye kundi la Mabaga freshi na walifanya vizuri sana kwenye game na kukubarika na mashabiki.


DTV INAWATENDEA HAKI WANAMUZIKI:DOGO ASLAY

Asema ni televisheni ya kizazi kipya ambayo haibagui msanii!
Na Livingstone Mkoi
Msanii chipukizi anaekimbiza kwenye muziki wa kizazi kipya nchini toka Tmk Dogo Aslay ameweka wazi ya moyoni mwake kwa kuipongeza televisheni ya DTV kwa kuwatendea haki wanamuziki wachanga kwa kupiga kazi zao na kuonekana.

Akiongea na Xdeejayz hivi karibuni katika viwanja vya Jangwani mwanamuziki huyo alisema kuwa "Naamini DTV inapaswa kupongezwa kwa kukubari kupiga kazi za wanamuziki wa aina yote bila masharti na kupelekea kuinua vipaji vyao" Alisema Dogo Aslay.

Monday, December 10, 2012

DTV IMEVUNJA REKODI YA JANGWANI JANA


Maelfu ya watu walio jitokeza jana katika viwanja vya jangwani ktk wakati wako tour ya DTV


Mkali dully akipiga show kwenye stage ya wakati wako tour ya DTV katika viwanja vya jangwani


Maelfu ya watu jangwani wakishuhudia show ya wakati wako tour ya DTV


Thursday, December 6, 2012

VITU VYA SHARO MILIONEA VILIVYOIBIWA NA KUKAMATWA KUZIKWA:KITALE!


Yaelezwa ni maagizo ya Mama mzazi wa Sharo,Vitu vitakavyozikwa ni pamoja spea taili,redio ya gari,beteri,saa ya mkononi,suruali aina ya jins pamoja na tisheti na begi. 
Na Mwandishi Wetu
Habari toka Mkoani Tanga nyumbani kwa marehemu Sharo Milionea aliyefariki mapema wiki iliyopita kwa ajali ya gari kisha vibaka kumporoa baadhi ya mali zake na baadae kukamtwa wakiwa na mali hizo familia ya hiyo imepanga kuvizika vitu hivyo.
Akiongea na wasanii wenzake Jumapili iliyopita Kitale ambae kwa sasa amechaguliwa na familia ya marehemu Sharo kusimamia baadhi ya majukumu aliyoaacha msanii huyo kabla ya kufariki.
Kitale aliyasema hayo alipokuwa kwenye kikao cha wasanii wa komedi kilichokuwa na mada ya nini cha kufanya baada ya msiba wa sharo pamoja na kufanya maandalizi ya arobaini ya Sharo"Mama wa marehemu ameagiza mali hizo kuzikwa ardhini na asingependa kuziona tena" Alisema Kitale
Hata hivyo Kitale aliendelea kusema uamuzi huo uliofanywa na mama wao huyo haukupingwa na ndugu yeyote na familia hiyo inajipanga siku ya kuzika vitu hivyo.

Wakati huo huo kuna taarifa kuwa kumezuka matapeli ambao wanajifanya ndugu wa marehemu kutaka michango ya kwa ajili ya kumsaidia mama huyo Kitale alisema hao wanajitafutia balaa kubwa kwani mama huyo ameshatoa onyo kwa mtu yeyote atakaejipatia pesa kupitia jina la Sharo cha moto atakiona.

AFYA YA MZEE MAJUTO SIO NZURI,WATANZANIA WATAKIWA KUMUOMBEA KWA MUNGU!

Kusafirishwa haraka toka Tanga kuja Dar kwa matibabu,Mtoto wake aongea na Xdeejayz na kuweka wazi ugonjwa unaomsumbua babake.
Na Livingstone Mkoi
Afya ya Mfalme wa Komedi Tanzania Amari Othuman Majuto”King Majuto”  ni ya mashaka baada kusumbuliwa na maradhi ya kuvimba miguu pamoja na shingo.
Akiongea mbele ya kikao cha wasanii wa Komedi Tanzania kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni na kushuhudiwa na mwandishi wetu mtoto wa muingizaji huyo aliyefahamika kwa jina la Hamza Amri Majuto alithibitisha taarifa za ugonjwa wa babaake.
Habari zaidi zilisema kuwa mzee Majuto anasumbuliwa  na kuvimba miguu pamoja na kuvimba shingo hali inayomfanya akose amani muda wote.
Mtoto huyo aliongeza kusema mzee wake amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa kipindi kirefu kidogo lakini alikuwa anatumia dawa za kawaida,Hata hivyo maradhi hayo sio ya kutisha sana kwani pia anajiweza kutembea mwenyewe kwa miguu yake hivyo ni hali ya kawaida.
Hamza ambae aliongea kwa ufupi alisema kuwa hali ndo hivyo babaake anahitaji dua ili apone haraka na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.