TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, November 24, 2012

HOSPITAL YA MWANANYAMALA YASHTUMIWA KUSABABISHA KIFO CHA MSANII WA BONGO MOVIEZ JOHN S. MAGANGA

 Msanii wa bongo moviez john s masanga amefariki dunia jana saa 4 usiku katika hospital ya mwananyamala kwa kile kilichosemakana kwamba alikuwa ameanguka ghafla katika semina aliyokuwepo kwa ajili ya mambo ya filamu.akiwa na kina natasha,mama yake monalisa na shija katika hali isiyokuwa ya kawaida ameanguka gafla,na kukimbizwa katika hospital ya mwananyamala hapo ndipo alipopimwa na kuambiwa kuwa alikua na vidonda vya tumbo  na kufanyiwa oparation, baada ya madaktar hao kuona kuwa hali yake imezidi kuwa mbaya wakamwamishia hospital ya muhimbili na huko ndipo alipoendelea kupata matibabu zaid, lakin hali yake ilizid kuwa mbaya na kugundulika kuwa alikuwa na ugonjwa mwengine tofauti na aliokutwa nao hospital ya mwananyamala.muhimbili waligundua kuwa alikuwa na ugonjwa wa kujaa maji katika mapafu. ambapo muda wa kutibia ugonjwa huo ulikuwa umeshakwisha mpaka kupelekea kifo chake. marehemu john s maganga ameacha pengo kubwakatika tasnia ya filamu tanzania,marehemu alishaigiza filamu nyingi kama;-mrembo kikojozi,chanzo ni mama, my dreams,cake ya birthday,bar maid,pretty gal. na nyingine nyingi.

 Marehemu john s maganga akiwa na shilole na zuhura gora enzi za uhai wake.

R.I.P  JOHN S MAGANGA



Wednesday, November 21, 2012

HAWA NDIO ASKARI WALIOUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA KUMUUWA RAIA SWETU FUNDIKIRA



Marehemu Swetu Fundikira

Baada ya kuahirishwa toka tarehe 30/102012 mpaka tarehe 20/11/2012 hukumu ya kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira leo asubuhi ilifikia tamati kwa Mh  jaji Zainabu Mruke kuwapata na hatia ya kumuua kwa makusudi Swetu Fundikira.

Jaji Mruke akisoma ushahidi wa pande ya mashtaka na ile ya utetezi alisema"Hakuna shaka kwamba hakuna mtu aliyeshuhudia(aliyeona) Swetu Fundikira akiuawa, hivyo katika hali kama hii ushahidi wa kimazingira ndio utakao pelekea kuthibitisha jambo hili pamoja na utetezi wa washitakiwa .
Lakini je, maelezo ya washtakiwa yanajitosheleza kuondoa shaka juu yao kuwa hawakuhusika na tukio hili? Katika hali ya kawaida hapa pana shaka kwa maelezo ya mshtakiwa wa pili Ali Ngumbe kwamba mtuhumiwa wa kwanza Rhoda alilewa hivyo hakuweza kuendesha gari hivyo ilibidi yeye(Ally) aendeshe kasha Rhoda arudi na gali hilo kutokea maeneo ya Ukonga airport hadi maeneo ya drive in ni dhahili kuwa jambo hili lilikua haliwezekani

“SHERIA:Melezo yasiyokidhi haja na yenye utata kwa upande wa ushahidi ni faida kwa upande wa mashtaka(Jamhuri)” Jaji alinukuu sheria
Pia kwa hali ya kawaida pamoja na kwamba hakuna aliyeona Swetu akiuawa lakini majeraha aliyokuwa nayo kichwani (marehemu) yanawafanya na kusababisha (washtakiwa) watoe maelezo na ushahidi wa kina bila kuacha shaka, jambo ambalo katika ushahidi wao limeonekana kutia shaka ya hali ya juu kuwa wao wamehusika na hali hiyo.
Ushahidi wa washitakiwa haukuweza kukata mnyororo wa mtiririko wa ushahidi hivyo kufanya mkono wa hatia kuwaelekea wao kuwa ndio walio sababisha kifo cha Swetu.
Ukirejea mtiririko wa ushahidi uliotolewa na mashahidi wote watano ambao umeweka mtiririko wa mnyororo ambao haukukatishwa na utetezi unatosha kuwa uthibitisho wa mauaji katika mahakama hii
MAZINGIRA YA KESI:
• Ushahidi umetengeneza mnyororo
• Ushahidi umeshindwa kutoa matundu
NIA OVU:
Katika kesi hii ya mauaji NIA OVU imethibiti katika mambo yafuatayo:
• Rhoda(mshitakiwa) alipotoa kauli ya kumwambia Sopstenes walipokuwa Mango kuwa “Usipoheshimu wakuu wan chi utaumia”
• Rhoda(mshitakiwa) alipotoa kauli ya kuwaambia wenzake kuwa “wale washenzi hawa hapa niliwaambia mwatie adabu mnaona sasa wametufuata mpaka huku?”
• Swetu kushambuliwa na watu watatu
• Watuhumiwa kujitambulisha kuwa wao ni wanausalama lakini hawakutenda jambo lolote la usalama
• Majeraha ya kichwani aliyokutwa nayo Swetu(a very sensitive area)
• Kumdhalilisha Swetu kwa kumuacha uchi wa mnyama
• Maneno ya washitakiwa kabla na baada ya tukio yalikua ni ya kijeuri na kikorofi wala hawakujutia kilichotokea.
Kwa maelezo haya haiwezekani kusema kuwa wamefanya jambo hili bila ya kukusudia(wameua kwa kukusudia)
Mheshimiwa Jaji aliomba kwa heshma na taadhima kutofautiana na wazee wote wa mahakama ambao wote kwa nmyakati tofauti wamekua wakitoa kauli za kuonyesha washtakiwa hawakukusudia na wamebambikiwa kesi kwa kusema kuwa wote watatu(washitakiwa) wamefanya/wamemuua Swetu Ramadhani Fundikira kwa kukusudia.
KOSA: Kosa limethibitika kwa ushahidi ambao hauna shaka hata kidogo kuwa washitakiwa wote watatu kwa pamoja wanahatia ya kumuu Swetu kwa kudhamiria:


WAKILI WA UTETEZI:
Kutokana na mazingira ya kesi hii naomba mahakama iwapunguzie adhabu wateja wangu kwa sababu kwamba wote ni vijana na wanahitajika katika ujenzi wa Taifa hili, wanategemewa na familia zao pia mazingira yenyewe ya kesi
Baada ya washitakiwa kuambiwa wamehukumiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia walipewa nafasi ya ya kusema neno lolote nao walisema mmoja mmoja kwa kuomba wapunguziwe adhabu.
Baada ya Jaji(Mh. Zainab Mruke) kuwasikiliza alitoa ufafanuzi kuwa pamoja na maelezo yote watuhumiwa wanapaswa kujua kua kuna nafsi imetolewa duniani kwa dhuluma (A SOUL HAVE BEEN LOST) na kama imethibitika mauaji ni ya kukusudia hukumu huwa ni moja tu kuuwawa ,akawaomba watu wate waliohudhuria mahakama kusimama na akatamka adhabu yao kuwa ni 

KUNYONGWA HADI KUFA TUNASHUKURU HAKI IMETENDEKA TENA KWA MUDA AMINA!

DVJ MAJEY NA HYPERMAN HK KUKIWASHA MTWARA ALHAMISS

The super duper hyperman man master hk alhamiss hii yeye na dj mkongwe dvj majay watakiwasha katika club ya kimataifa iliyoko mkoani mtwara inayokwenda kwa jina new maisha club mtwara akiongea na xdeejay mratibu wa tour hiyo iliopewa jina la triple bash hemed kavu hk alisema kila mwenzi tutakuwa na event katika club zote tatu yaani dodoma,mtwara na dar za maisha club. kupitia udhamini wa nmb na kilimanjaro primium beer. kwa mwenzi tunapita mara moja kwenye kila club lengo ni kuto aburudani tofauti kabisa na walioizoea.alhamiss hii tutakuwa mtwara wikiend dododma na tar 8 tutakuwa dar.

Thursday, November 15, 2012

ZILIZOINGIA SOKONI WIKI HII KWENYE BONGO MOVIES









MWILI WA MAREHEMU MARIAM KHAMIS WAZIKWA NA MAMIA YA WATANZANIA

 

SAA 10 jioni leo kama ilivyotangazwa hapo awali, mwili wa Marehemu Mariam Khamis ulizikwa katika makaburi ya Ndugumbi, Magomeni jijini Dar es Salaam.Maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza kwenye mazishi ya mwimbaji huyo nyota wa miondoko ya muziki wa taarab huku kila mmoja akiwa ametandwa na uso uliojaa huzuni.

Mume halali wa marehemu Mariam Khamis, Haji Kijungu ambaye ni mpiga bass wa Super Shine Taarab alikuwa ni mmoja wa watu waliowatia watu simanzi msibani hapo hasa kutokana na ukweli kuwa katika kipindi cha mwisho cha uhai wa marehemu, wawili hao hawakuwa wakiishi pamoja.


 Mwili wa marehemu MARIAM KHAMIS ukipelekwa makaburini.

 Ndugu,jamaa na marafiki wakikaa kwa huzuni msibani


jeneza la  marehemu mariam khamis

Wednesday, November 14, 2012

LEVICIOUS JONSON MWANAMITINDO WA KIMATAIFA ANAETAMANI UHUDUMU WA KWENYE NDEGE!

 Mwanamitindo nyota toka Mkoani KilimanjaroTanzania  Levicious Jonson akiwa kwenye picha ya pozi.
 Mwanamitindo Levicious Jonson "18" katikati akiwa na wanamitindo wenzake.

 Mwanamitindo  Levicious Jonson akiwa kwenye picha ya pozi na mwanamitindo mwenzake.

 Mwanamitindo  Levicious Jonson  Kulia akiwa kwenye picha ya pozi na mwanamitindo mwenzake.
 Mwana mitindo nyota toka Mkoani Kilimanjaro Levicious Jonson(18) amejitokeza na kuweka wazi malengo yake ya kuja kuwa mhudumu wa ndege na huku akiwa mwanamitindo maarufu.


Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu toka Moshi Mwanamitindo huyo alisema kuwa anahitaji kujweka bize sana kwa mwaka 2013 ili afanikishe masomo yake ya uhudumu wa ndege" Unajuwa nini kimsingi nimejipanga kufanya vyema masomo yangu ya uhudumu wa ndege bila kuathiri fani yangu ya  " Alisema Levicious Jonson

Hata hivyo Levicious Jonson aliongeza  kusema kuwa kazi ya uana mitindo ameianza miaka mitatu iliyopita na imempatia mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukutana na watu maarufu barani pia imempa uzoefu mkubwa nk.

Aidha mrembo huyo mwishoni mwa mwezi huu anatarajia kuja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa Mkoa wa Kilimajaro pamoja na kazi za unamitindo zinavyoweza kuitangaza Tanzania hasi ikitegemea kuwa mkoa wa Kilimajaro unautalii wa kihistorie kuliko Mkoa mwingine wowote Tanzania.