TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Sunday, May 29, 2016

MSANII AFANDE MACHEMBA AWACHANGANYA MASTAA WA KIKE BONGO MOVIE, YUPO CHUCHU HANSI. RAY MMH MAJANGA MATUPU...!



 AFANDE MACHEMBA AKIWA MZIGONI NA CHUCHU HANS, AMBAPO MSANII HUYU WA KIUME AMEONEKANA KUWA NA NYOTA YA AJABU KWENYE TASNIA YA BONGO MOVIE KUTOKANA NA KIPAJI CHA HALI YA JUU ALICHOKUWA NACHO.

 Ray na Chuchu
 
Na Mwandishi Wetu
Kitendo cha mastaa mbalimbali wa filamu Tanzania kutaka kufanya kazi pa1 na msanii chipikizi anaekuja kwa kasi ya kimbunga kwenye tasnia hiyo Joseph Machemba " Afande Machemba" kimeendelea kumuweka kwenye wakati mgumu msanii huyo.
Akiongea na maskanibongotz Machemba alisema " Kaka hakika Mungu ni mwema na sijui nimpe nini huyu Mungu wangu kwa matendo yake makuu hadi nashangaa kwa baraka zake ambapo licha ya uchanga wangu kwenye tasnia hiyo lakini napata kazi kubwa ambazo zote naigiza na mastaa ambao kiukweli hakuna asiyekubari kazi yangu" Alisema Machemba
Msanii huyo ambae ni msukuma wa Shiyanga aliongeza kusema hali hiyo ya kupata kazi kila siku imemfanya kuwa busy na uigizaji kiasi cha kukataa kazi za watu wengine kutokana na ratiba inavyombana.
Afande Machemba aliendelea kueleza kuwa hadi sasa ameshacheza filamu nyingi na tayari mlango wa mafanikio ameanza kuuona " Kaka msema kweli mpenzi wa Mungu tayari nimeanza kuonja mafanikio ya sanaa nilianza kucheza filamu bure lakini kwa sasa nalipwa tena naweza kusema hela ndefu, nina washukuru wasanii wenzangu hasa mastaa wote hakuna ambae hanikubari kila filamu natakiwa nishiriki" Alisema msanii Machemba hadi sasa ameshacheza filamu nyingi sana ikiwemo Chobo Dundo, Smart Phone, Handsome Fake, na nyingine ambazo zote zipo madukani na yeye akiwa ametumia jina la Afande Machemba.