TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, February 10, 2016

KIMENUKA: DC MAKONDA AHUSISHWA NA MAUAJI YA KUTISHA, WANANCHI WAPANGA KUFANYA MAANDANO MAKUBWA, WAMCHONGEA KWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI, MASKANIBONGOTZ INAKUPA ISHU NZIMA...!

Huyu ni mmojwa aliyekuwa baunsa maaarufu aliyefahamika kwa jina la CHURA kabla ya kufikwa na umauti akiwa Hospital ya Mwananyamala baada ya kukatwa katwa mapanga kichwani eneo la tukio.
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Wakazi zaidi ya elfu 5000 wa kata ya Wazo mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa juzi walifanya kumbukumbu ya kuwakumbuka marehemu wote waliorafiki kwenye migogoro ya ardhi kwenye mtaa huo huku wananchi hao wakimuhusisha  Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kuwa kama angekuwa tayari mkuu wa Wilaya basi mauaji hayo yasingetokea leo hii.
Wakiongea na mtandao huu wa habari za uchunguzi wananchi hao walisema " Kiukweli tunawakumbuka ndugu zetu waliopoteza maisha wakiwemo wale mabaunsa waliopigwa mishare ya kichwa na mapanga kisa mgogoro huu wa ardhi ambao kwa sasa Mheshimiwa Makonda anakwenda kuumaliza na tunaamini kama Mheshimiwa Makonda angekuwepo hakika hakuna tone la damu ambalo lingemwagika" Walisema

Hata hivyo   wananchi hao wameendelea kumuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kumuongezea majukumu DC Makonda kwa kumpa ukuu wa Mkoa kwani kwa sasa ndiye DC pekee anaefanya kazi usiku na mchana huku mafanikio yake yakionekana  hali inayopelekea hata Wilaya nyingine za Jiji la Dar wakihitaji msaada wake.

Hata hivyo licha ya zoezi la uhakiki kubakisha wiki mbili kumalizika, lakini kwa sasa limesimama kidogo kufutia kuwepo kwa mtafaruku wa kati ya mtu aliyedai kuwa hilo shamba lake ambae ilifahamika kama alishaliuza kwa muhindi huku RC na DC Lugimbana wakidaiwa kuwa mashahidi wa mauziano hayo, hivyo kwa sasa eneo hilo lipo chini ya muhindi lakini cha kushangaza muhindi amegoma kujitokeza badara yake amekuja mtu aliyeuza tayari eneo hilo huku kamati za ardhi kata hiyo zikifahamu fika kama huyo mtu eneo hilo halimuhusu tena.
Aidha wakazi hao ambao wengi wao ni wakina mama wanasema wanampango wa kufanya sherehe kubwa ya kumpongeza DC Makonda kwa kazi nzuri ya kutenda haki aliyoifanya bila kuogopa nguvu ya mafisadi lakini pamoja na kigogo mwenye mamlaka kuliko yeye ambae anadaiwa kwenye mgogoro huo anamkono wake.

Sunday, February 7, 2016

ANGALIA MECHI YAKE YA KWANZA YA MBWANA SAMATTA AKIWA NA KRC GENK YA UBELGIJI...!


Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea tena leo February 6 kwa michezo kadhaa kupigwa, miongoni mwa michezo iliyochezwa leo February 6 ni mchezo kati ya Mouscron FC dhidi ya klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, mchezo huu ulikuwa na mvuto kwa Tanzania zaidi kwani ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta kucheza toka amejiunga na klabu hiyo.
moegnk
Mbwana Samatta ambaye ndio nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya KRC Genk akitokea benchi, Samatta aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya  Nikolaos Karelis ambaye alitoa pasi ya goli la ushindi kwa KRC Genk dakika ya 63 na Thomas Buffel kupachika mpira nyavuni.
s
Mchezo ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji wao Mouscron, lakini hadi mpira unamalizika Mouscron walikuwa wanaoongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 53 na KRC Genk asilimia 47, ushindi huo umeifanya KRC Genk kutimiza jumla ya point 38 na kusogea hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi. KRC Genk wanarudi tena dimbani February 13 kucheza dhidi ya Waasland-Beveren katka dimba lao la Cristal Arena.
we
sw
sda
ass
1

Saturday, February 6, 2016

UKAWA DAR WAMPIGIA SALUT DC MAKONDA, WAMTAKA AGOMBEE UBUNGE KUPITIA CHAMA CHOCHOTE WATAMPIGIA KURA ZA KUMWAGA, MASKANIBONGOTZ INASHUKA NAYO.....!

DC MAKONDA KATIKATI AKIWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA MH MBOWE HIVI KARIBUNI KWENYE MAJUKUMU YA KITAIFA.

Na Mwandisahi wa Maskanibongotz
Wafuasi wengi wa Ukawa Kinondoni Jijini Dar wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na ufisadi na kuwa mtetezi wa wanyonge hasa kwenye suara la migogoro ya 
ardhi.
Wakiongea na maskanibongotz  wafuasi hao walianza kusema kuwa" Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Makonda ni kiongozi anaehitajika kwa watanzania na hata hivyo sijui kwa nini mheshimiwa Rais alichelewa kumteua huenda hata watu wasingepoteza maisha kule Nyakasangwe" Walisema watu hao
Hata hivyo wananchi hao waliongeza kusema kuwa Makonda angepewa Ukuu wa Mkoa wa Dar ili amalize matatizo ya ardhi kabisa kwani hata wilaya nyingine za Jiji la Dar zinamuhitaji kwani alichokifanya Wazo kwenye mtaa wa Nyakasangwe hakika anastahiri pongezi ikizingatia viongozi wengi akiwemo Mkuu wa Mkoa Meck Sadick walishindwa kumaliza tatizo hilo.
Aidha wananchi mbalimbali walitamani hata DC huyo kugombea ubunge Jimbo la Kawe ama Kinondoni ili akapaze sauti yake bungeni.

Friday, February 5, 2016

AFANDE MACHEMBA AWAAMSHA USINGIZINI RAY NA JB, MASHABIKI BONGO MOVIE WAWATAKA MASTAA HAO KUSTAAFU SANA KUPISHA DAMU CHANGA...!

 AFANDE MACHEMBA

WASANII WENYE MAJINA NCHINI TANZANIA BONGO MOVIES TEAM




Na Mwandishi wa Maskanibongotz

Kipaji cha Msanii kinda kwenye tasnia ya Filamu Tanzania Joseph Machemba sasa kimeonekana kuwaamsha uzingizini mastaa wa kiume Vicent Kigosi"Ray" Na Jakobu Steven "JB" na wengine huku mashabiki wengi wakiwashauri Ray na Jb kuachana na sanaa kwa sasa.

Mashabiki hao wakiongea na maskanibongotz walisema kwa kipaji anachokionesha msanii Afande Machemba  hakika ni dhahiri kabisa anaweza kuifikisha sanaa ya Tanzania Kimataifa na sio kama Ray na Jb ambao kwa sasa wanasafiria nyota za zamani kwa kushindwa kufanya juhudi zozote za kuwa wa kimataifa.

Mashabiki hao waliendelea kusema wamefurahishwa na upinzani mkali aliouonesha  Afande Machemba kwenye sanaa kwani kulizika kwa msataa walipo kungeweza kuleta athari kwenye sanaa hii kwani Ray na Jb uwezo wao ulishakufa tangu alipotangulia mbele za haki Marehemu Steven Kanumba hadi leo sanaa ya Filamu imerudi nyuma kwani hakuna hata staa mmoja ambae anaonekana ana kiu kama aliyokuwa nayo marehemu Kanumba ya kuifika sanaa ya Tanzania kimataifa.

Filamu zilizomtambulisha Afande Machemba ni Filamu alizoonekana Afande Machemba ni pamoja na, Karoge  Tena, Night Dress, Akiri Nyingi, Bifu la Kitongoji na ndani yake ameonesha kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwafanya mashabiki wanajiuliza kwa nini alikuwa amechelewa kuanza kuigiza.

Thursday, February 4, 2016

MUNGU AZIDI KUONESHA MAAJABU YAKE NDANI YA KANISA LA MCHUNGAJI MWENYE NGUVU YA KIPEKEE, MAMIA YA WATU WAZIDI KUMIMINIKA , WAGONJWA WA UKIMWI, WASIOPATA WATOTO SASA WABEBA MIMBA, NI MAMBO YA KUSHANGAZA KWELI..!

Hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Kanisa la Sayuni lililopo Nyakasangwe Kata ya Wazo, ambapo kutokana na uponyaji wa kweli unatendeka Kanisani hapo mamia kwa mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi ili kupata uponyaji wa kweli. Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Mzola ameendelea kuwataka watanzania kuendelea kufika Kanisani hapo kwa ajiri ya kupata uponyaji wa papo kwa hapo.


Mrs Mzola akiwa kwenye ibada

Ndani ya Kanisa hilo uponyaji hufanyika wa papo kwa hapo bure bila malipo

 Mchungaji Mzola

Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Katika hali ya kushtua baada ya kuvuja kwa taarifa za Kanisa linalotibu mardhi ya aina yote huku Mungu akimtumia mtumishi wake Mch Mazola kufanya hayo yote  maelfu ya watu wameendelea kumiminika Kanisani hapo kiasi cha kukosekana nafasi ya kukaa kwa ajiri ya kupata uponyaji wa bure.
Mchungaji huyo akiongea na gazeti la Maskani Bongo alisema" Kiukweli tunamshukuru Mungu Muumba mbingu na ardhi kwa baraka zake toka habari ziwafikie watu wake basi wamekuwa wakimiminika usiku na mchanga kuja kupata uponyaji wa kweli" Alisema mchungaji huyo
Mchungaji huyo aliongeza kusema kuwa anaendelea kutoa uwito kwa watanzania wote kuendelea kufika Kanisani kwake ili wapate uponyaji, kwani Kwa Mungu hakuna lisilowezekana, kila magonjwa yote sugu, ugumba, utasa, mikosi ya kushindwa kuolewa/kuona, kuwa na mashaka, hofu ya kifo nk.
Na amesema watkaoshindwa kufika kanisani kwake Kata ya Wazo mtaa  Nyakasangwe wanaweza kumpigia simu kupitia namba hizi 0763-161785/ 0713-161785 na wao watapokea uponyaji huko walipo.