TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, March 30, 2015

KASHFA NZITO HOSPITALI YA SINZA PALESTINA WAMUUA MTOTO KWA UZEMBE, MGANGA MKUU ACHANGANYIKIWA ASEMA YUPO TAYARI KUWAJIBISHWA KWA TUKIO HILI. WAZIRI WA AFYA AOMBWA KUSIKITISHA VIKAO VYA BUNGE NA KUUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI..!

KUMRADHI KWA PICHA HII: Maskani ya Mungu huyu ndiye mtoto aliyepoteza maisha kwa ezembe wa  Manesi wa Hospital ya Palestina  

 Mama mzazi akihojiwa na Kitengo Maalum Cha Habari za Uchunguzi cha E-fm Radio
Mwandishi wa toka Kitengo Maalum cha habari za Uchunguzi Bw Livingstone Mkoi akisoma kwa umakini vyeti alivyokuwa amepewa mama huyo mara baada ya kuruhusiwa kwenye Hoisptali hiyo ya Palestina


Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Pinda ambae amehusishwa na tukio hili kwa kuombwa na watanzania kuamuru kuundwa kamati ya uchunguzi kutokana na tukio hilo la kifo cha mtoto huyo asiyekuwa na hatia
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid ameombwa kukatisha vikao vya Bunge Mkoani Dodoma na kurudi Dar kwa ajili ya sakata hili ili wananchi wawezi kurudisha imani kwa Serikali yao.

Mbunge wa Ubongo Mh John Mnyika.



Na Livingstone Mkoi Mwandishi  Habari za Uchunguzi wa

E-FM Radio

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua hospitali ya Sinza-Palestina imekumbwa na kashfa nzito ya kusababisha kifo cha mtoto mchanga baada ya kutokana na uzembe wa hali ya juu.

Habari zaidi toka kwa mama mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Kimaro, mwenye miaka 40, zinadai kuwa, tarehe 22 mwezi huu (Machi) alishikwa na uchungu majira ya saa tisa usiku na asubuhi kulipokucha mdogo wake aliyefahamika kwa jina la Msiyaka alimpeleka hospitali hiyo ya Palestina kwa ajili ya huduma zaidi.”

Akisimulia kwa majonzi makubwa, mama huyo ambaye ni mkazi wa Mabibo aliendelea kusema kuwa, akiwa hospitalini hapo, baada ya kupokelewa na madaktari, alipimwa na kumwambia kuwa, hana tatizo lolote na kwamba alielekea kujifungua bila shida  huku wakimsisitizia kuwa njia inafunguka vizuri japo alikuwa amekaa muda mrefu bila kuzaa.

Akaendelea kusimulia kuwa, baada ya kumaliza kumpima, mama huyo anadai akaendelea na mazoezi mepesi kusubiri mtoto ashuke na ilipofika muda wa saa tatu usiku, kuna wahudumu waliokuwa wamempokea tangu asubuhi muda wao ulikuwa umekwisha, wakaondoka na yeye alikabidhiwa kwa dada mwingine mhudumu wa zamu ya usiku.

Hata hivyo, mama huyo anasema wahudumu wa zamu ya mchana walikuwa na moyo wa kibinadamu na huruma ya hali ya juu kwani aliwaona wakipigania kuokoa maisha ya akina mama na watoto wao huku akiwataja majina ya Elizabeth na Hyasinta.

Mama huyo anasema wahudumu walioachwa zamu ya usiku ni watoto wadogo wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 18 na 20 na ndio walionekana mara moja kuzungukazunguka kwenye wadi ya wajawazito (leba) kuwahudumia waonasubiri kujifungua huku leba hiyo ikiwa haina umeme kabisa.

Aidha, mama huyo aliendelea kueleza kwa uchungu kuwa, wakati hayo yanaendelea, wahudumu watu wazima walikuwa wamekaa upande wa pili wakinywa kahawa na kutafuna kashata licha ya yeye kuwaita mara kwa mara, lakini, aliishia kujibiwa; “Wewe unapiga kelele tangu umefika hapa, unaitaita tuuu, kwani mtoto ameshatoka tayari?”

Mama huyo alizidi kusema kuwa, baada ya kuona amezidi  kupiga kelele za kuomba msaada kutokana na mtoto kuanza kushuka, mkuu wa wahudumu hao alimtuma mhudumu mmoja binti aende kumtazama na baada ya nesi huyo kufika alimwambia kuwa kama taa hakuna basi achukuke simu yake ya mkononi atumie tochi imsaidie kumtolea mkojo uliokuwa umembana sana.

Hata hivyo, nesi huyo kijana alipochukua simu hiyo ili akachukue mpira na kurudi kwa kutoa mkojo, kabla hajamtoa mkojo, tayari mtoto alikuwa njiani kutoka na ilibaki kusukuma tu na mtoto alikuwa mzima, lakini, alikuwa amechoka kutokana na kukaa muda mrefu kwani mtoto ilikuwa azaliwe saa tatu lakini amezaliwa saa tano na dakika kadhaa.

Mama huyo anaendelea kusema, alikuwa kila akiwaeleza manesi  wamsaidie, walimwambia ajigeuze tu, hata ubavu, kwa vile mtoto alikuwa anatoka, huku wao wakimalizia kwa vicheko vya kejeli.

Kadhalika, mara ya pili yule nesi aliporudi alichukua tochi ya simu yenye mwanga kwani wao hawakuwa na simu zenye mwanga mkubwa (smart phone) na baada kufika kwa huyo mama, tayari mtoto alikuwa kishazaliwa.

Elizabeth hapa anasema, kwa kweli hili hata akiitwa kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid atasema hata kwa kuapishwa kwa kitabu cha imani yake baada ya yule mhudumu kufika pale na kukuta mtoto amezaliwa huku akiwa amechoka, alimuokota mtoto na kumuingiza mipira puani kwa nguvu, basi hapo damu nyingi kama bomba zilianza kumtoka mtoto puani na yule mhudumu alivyoona hali ile alishtuka na kusema; ‘Mungu wangu’.

Baada ya hapo mhudumu huyo alichukua khanga na kumwambia eti ngoja ampeleke sehemu ya mwanga huku damu zikiendelea kulowesha khanga na baada ya kumpeleka mtoto huyo mhudumu huyo alirudi tena na ile simu yake akiendelea kusaidia akina mama wengine na hakuhangaika naye tena licha ya kuhitaji msaada wa kukamuliwa damu tumboni ili kutoa uchafu.

“Yaani sikupata msaada wowote, yule binti nesi aliendelea kuhangaika mwenyewe usiku mzima kwa kuwazalisha akina mama wajawazito wengine,” analalamika Elizabeth.

Hata hivyo, mama huyo anasema kumbe kipindi mwanae alikuwa ameshapoteza maisha wala wasimwambie, lakini, cha kushangaza ni baadae aliwaona wahudumu kama watano wakiwa ‘bize’ na wagonjwa akajiuliza kumbe wahudumu wote wapo iweje akina mama wapate shida kiasi kile hata kusababisha watoto kupoteza maisha?

Mama huyo anasema, licha ya uzembe wa wahudumu kusababisha kifo cha mtoto wake, lakini, pia lawama nyingine anazipeleka moja kwa moja kwa uongozi wa hospitali kwa kushindwa kuweka umeme hata wa dharura katika ‘leba’ ikizingatiwa ni mahala muhimu kuwa na umeme wakati wote.

Aidha, mama huyo anadai kuwa, alipomaliza wahudumu hao walimjibu: “Hili ni tatizo la muda mrefu, hii ndio serikali yenu,   kwanza hospitali hizi hazina vifaa, someni ubaoni walivyoandika wenyewe kwa uzembe wao, hairuhusiwi kwa mama yeyote mjamzito kutoa rushwa, eti, vitu vyote ni bure! Uchungu nao ni shilingi ngapi? Eti tusaidiane!!!”

Mama huyo anasema baada ya mwanae kupotea mhudumu huyo alikuja kumuweka wazi kuhusu kifo cha mtoto na alipomuhoji  sababu ya mwanae kufariki, mhudumu aliongopa kuwa eti mtoto wake alizaliwa akiwa amejisokota shingoni jambo ambalo hakubaliani nalo kwa kuwa kwake haikuwa mara ya kwanza kuzaa na hata walipokabidhiwa mwili wa mtoto huyo haukuwa na alama ya kamba kujisokota zaidi ya damu nyingi puani.

Kufuatia tukio hilo, licha ya mama huyo ambaye ni mfuasi wa ulokole kutaka kusamehe suala hilo, familia yake imemkatalia mama huyo na kusema watafika nalo mbali ili kukomesha ukatili unaoendelea kwenye hospitali hiyo. Aidha, kutokana na mama huyo kuwa katika hali ambayo haijatengemaa kutokana na kifo cha mwanae, alipandwa na presha na hadi sasa bado hali yake ni mbaya.

Nacho kituo cha E-FM Radio 93.7 kupitia kwa Kitengo Maalum cha Habari za Uchunguzi, hatua ya awali kimepiga hodi kwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dokta Luoga ambaye  ameshtushwa na tukio hilo kwa vile alikuwa amepewa ripoti tofauti juu ya kifo cha mtoto huyo na wasaidizi wake.

“Jamani, haya mbona makubwa, taarifa za kifo cha mtoto huyo hizi mezani kwangu, lakini, ziko tofauti na haya maelezo ya huyo mama,” alisema Dokta Luoga ambaye kipindi hicho alikuwa akisikilizishwa sauti ya mama huyo iliyorekodiwa.

Aidha, mganga huyo baada ya kuandika maelezo hayo, aliitisha kikao cha dharura na wakuu wa hospitali hiyo wakiwemo wale wa Ustawi wa Jamii na kusikiliza tuhuma hizo na kuchukua maelezo ambapo maganga huyo alisema kuwa, apewe muda wa siku mbili tatu afanye uchunguzi kisha atatoa taarifa ya kiofisi na kama hata yeye atakuwa amehusika kwa uzembe wa namna yoyote yupo tayari kuchukuliwa hatua na kama ikibainika wasaidizi wake ndiyo chanzo basi atamuomba Waziri mwenye dhamana kuchukua hatua kali za kinidhamu dhidi yao.

Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wadau wa hospitali hiyo pamoja na wananchi wameiomba serikali kupitia Waziri wa Afya kuchukua hatua kali za kisheria wote waliohusika na uzembe wa kifo cha mtoto huyo pamoja na wale wanaokula rushwa kwa wagonjwa kwani pia, tukio hili limehusishwa na rushwa ambapo E-FM ina taarifa zaidi juu ya tuhuma hizo za rushwa kwa baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo.

Pia hata Mheshimwa Waziri Mkuu amehusiswa  kwenye ishu hii na kuombwa kuamliwa kuundwa kamati ya uchunguzi kuhusu uzembe wa kifo cha mtoto huyu na wale wote watakaobainika wamehusika basi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja kufukuzwa ili iwe fundisho wa wahudumu wengine watakaobaki.

Wakati huohuo, Elizabeth, licha ya kupoteza mtoto wake, amesema anamuomba hata Waziri wa Afya awaongezee mishahara manesi aliowataja awali (Elizabeth na Hyasinta) kwa utendaji na uwajibikaji wao mzuri wa kazi kwani hata walipokuwa wanaondoka waliwaaga wagonjwa kwa kuwafariji na kuwatia moyo hali iliyowafanya baadhi ya wagonjwa kusikitika kwa kuondoka kwao.

Hata msimamo wa familia kuhusu tukio hilo imesema kuwa kwa sasa bado wanamuhangaikia mama huyo kwani hali yake bado ni mbya kufuatia kupatwa na mshtuko kuhusiana na kifo cha mtoto wake ambapo licha ya kwamba alikuwa na matatizo ya pressure na hili ndo limemuongezea hali hiyo na mara baada ya kupata nafuu basi wako tayari kulifikisha mbali suala hilo ikibidi hata kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete watafikisha kilio chao.

Hii ndiyo sehemu ya kwanza ya taarifa hii ya kusikitisha lakini bado tutaendelea kuwataarifu hatua kwa hatu kwani Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dokta Luoga ambae ameomba kupewa muda wa kulifanyia uchunguzi wa kina na kubaini usiku ule ni wahudumu gani walikuwepo pamoja na mkuu wao manesi kasha atatoa taarifa za hatua zinazostahiri kuchukuliwa dhidi yao.

Pia E-fm Radio 93.7 kupitia kitengo maalum cha habari za uchunguzi na ndiyo waliovumbua skendo hii ya kusikitisha inaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Waziri wa Afya kwa ili kumfikishia taarifa za Skendo hii pamoja ushahidi mwingine, lakini shukrani za pekee zimuendee Mwandishi Mkuu wa Kitengo hicho cha Habari za Uchunguzi ndani ya kituo cha E-fm Radio Bw Livingstone Mkoi ambae amelifatilia suala hili usiku na mchana kuhakikisha ushahidi unakamlika hadi habari hii inaruka hewani. Source: E-fm Radio


Monday, March 23, 2015

NAS B AZUSHA BALAA JIJINI DAR WANAMUZIKI WAMFANYIA FUJO STUDIO KWAKE, AZIDI KUPUNGUZA GHARAMA ZA KUREKODI...!

Studio mpya ya PAMOJA RECORD kama inavyoonekana baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa studio hii inapatikana Magomeni Mapipa...!

 
  Prodyuza na Mwanamuziki Nas B akiwa pamoja na mwanamuziki Smat Boy

Na Mwandishi Wetu
Prodyuza na mwanamuziki mwenye kipaji Nas B amezusha balaa kubwa studio kwake baada ya kutangaza kuwasaidia wasanii wachanga kurekodi kwa gharama nafuu, hata hivyo hatua hiyo imezusha balaa kubwa kufuatia mamia ya wanamuziki kuanza kumiminika wakihitaji kutumia fursa hiyo kufanikisha malengo yao.
Akiongea na mtanda huu Nas B alisema' Imekuwa shida sana tangu tutangaze kuwepo kwa punguzo la beo kwa wanamuziki hatimae wanamuziki wamekuwa wakimiminika balaa na hali hiyo inanifanya kukesha usiku mzima ili kuwafanyia kazi zao" Alisema Nas B anaetamba na kibao chake cha Mademu wa Wasanii
Aidha Nas B aliongeza kusema kuwa anatoa uwito kwa wanamuziki kuendelea kutumia nafasi hii kufika studio kwake kwa ajir ya kurekodi na ofa hii itaisha mwezi wa nne na hatua hiyo ilikuja baada ya prodyuza huyo kutengeneza studio zake na kuwa za kisasa na ametumia gharama zaidi ya milioni 50 kukamlisha vifaa vyote.
Wanamuziki wa injili, bongo flava, nyimbo za asili wote mnakaribishwa na waliotayari wampigie kutumia namba 0714-595432 watampata moja kwa moja. " PAMOJA RECORDS INAKUPA NAFASI YA KUTIMIZA NDOTO ZAKO"

ARUSHA KWA WAKA MOTO MCHEZO WA RUGBY, WANAFUNZI ZAIDI YA MIA SITA WAJITOKEZA KUSHIRIKI MCHEZO HUO HATARI DUNIANI...!


Mchezo wa rugby uliendele kanda ya kaskazini ya Tanzania ikijumuisha mashule Nane kutoka mikoa Arusha Mjini Moshi na Monduri ambapo timu ziligawanyika kutokana na umri wa U9, U12, U14 ambapo kila group lilikuwa na timu 10 ambapo mpaka fainal timu za kutoka timu za Shule Mageleza walikuwa wa kwanza wapili walikuwa timu kutoka Meru wakiwa wapili na Makumbusho wakiwa washindi wa tatu Huu ulikuwa mwanzo wa kuwa kutanisha mashule yote pamoja ambayo yalijumuisha wanafunzi 600 toka Shule 8 Mwamko ni mkubwa sana Watoto wanaonyesha kuukubari mchezo wa raga upande wa kaskazini




Saturday, March 21, 2015

MANAIKI SANGA SASA SIFA AWASHUSHA WANAMUZIKI AZONTO NA SHUMBA RATSHEGA KUSHIRIKI FILAMU YAKE MPYA






 Washiriki wa filamu mpya ya Manaiki Sanga iitwa Wake Up ambao ni mastaa wakiwa mbele ya camera
  Miss Temeke Irine Kanka ambae aliwahi kudaiwa kutoa mimba 2 za Manaiki huku picha hizi zikizusha balaa kubwa kiasi cha dada huyo kuachwa na mchumbaake
  Mrembo toka Kenya akiwa kwenye mahaba na Manaiki Sanga
  Madam Wema akiwa chini ya ulinzi wa Manaiki Sanga
 Picha zilizowahi kuleta utata kwenye jamii hapa Manaiki na Uwoya wakiwa kwenye mahaba mazito

 Mwanamuziki Azont akiwa na Msanii Manaiki Sanga

 Filamu ya kwanza ya msanii Maniki Sanga iitwayo NGEMA

Manaiki akiwa shabiki wake ambae ni mwanamuziki toka kundi la MKUBWA NA WANAE
 Manaiki Sanga akiwa na shabiki wake
 Kiongozi wa kundi la Makhirikhir la nchini Botswana Shumba Ratshega

Na Mwandishi Wetu Msanii wa bongo movie nchini Manaiki Sanga sasa ameanza kulewa sifa na kuwahenyesha mastaa wa bongo movie kufuaita kuwaleta mastaa mbalimbali toka nje ya nchi ili kuja kushiriki filamu yake nyingine baada ya ile ya Wake Up aliyowashirikisha mastaa zaidi ya Hamsini. Kwa mujibu wa Manaiki Sanga mwenyewe aliuambia mtandao huu kuwa wakati filamu yake ya ikiwa bado ipo hatua za mwisho kuachia sokoni baada ya kufikia makubaliano na kampuni ya usambazaji ya Steps sasa anaingia tena msituni kurekodi filamu nyingine. Manaiki Sanga aliendelea kusema kuwa filamu hiyo ambayo itachezwa na wanamuziki kama Azonto toka nchini Uingereza na kiongozi wa kundi la Makhirikhiri toka nchini Botswana na mwanamuziki toka nchini Kenya Jaquar na hapa nchini watachukuliwa msanii Jakob Steven, Wema Sepetu, King Majuto, Lulu Michael, Zigamba na Mzee Majuto. Manaiki ambae amewahi kuitisa dunia kwa picha zake za aibu kwa wanawake zaidi ya 800 aliotembea nao tena bila kondom wakiwemo mastaa wakubwa wa bongo movie pamoja na mtoto wa familia ya Rais wa Zanzibar.
MANAIKI SANGA AZIDI KULEWA SIFA AWASHUSHA WANAMUZIKI AZONTO NA SHUMBA RATSHEGA KUSHIRIKI FILAMU YAKE MPYA Posted by maskani bongo at 12:17 AM MSANII MANAIKI SANGA AKIWA SHABIKI WAKE KIONGOZI WA KUNDI LA MAKHIRIKHIRI TOKA NCHINI BOTSWANA SHUMBA RATSHEGA AKIWA NA MSEMAJI WAKE HAPA NCHINI TANZANIA BW LIVINGSTONE MKOI. MANAIKI AKIWA KAZINI KWENYE MOJA YA MOVIE ZAKE MSANII MANAIKI SANGA AKIWA NA MWANAMUZIKI TOKA GHANA NAEISHI NCHINI UINGEREZA. FILAMU YA KWANZA MANAIKI SANGA IITWAYO NGEMA ILIYOWAHI KUMPA UMAARUFU MKUBWA NCHINI MSANII MANAIKI SANGA AKIWA NA MASTAA WENZAKE MSANII MANAIKI SANGA AKIREKODI FILAMU YAKE MPYA IITWAYO WAKE UP AMBAYO BADO HAIJATOKA MSANII MANAIKI SANGA AKIWA NA IRENE UWOYA FILAMU YA NGEMA JINSI ILIVYOSHENI MASTAA MBALIMBALI WASANII WALIOREKODI FILAMU YA NGEMA HEMED NA IRENE UWOYA MSANII MANAIKI AKIWA NA SHABIKI WAKE AMBAE NI MWANAMUZIKI TOKA KUNDI LA MKUBWA NA WANAE MASTAA WA KIKE BONGO MOVIE AMBAO WAMEONESHANA KAZI KAZ KWENYE FILAMU YA NGEMA Na Mwandishi Wetu Msanii wa bongo movie nchini Manaiki Sanga sasa ameanza kulewa sifa na kuwahenyesha mastaa wa bongo movie kufuaita kuwaleta mastaa mbalimbali toka nje ya nchi ili kuja kushiriki filamu yake nyingine baada ya ile ya Wake Up aliyowashirikisha mastaa zaidi ya Hamsini. Kwa mujibu wa Manaiki Sanga mwenyewe aliuambia mtandao huu kuwa wakati filamu yake ya ikiwa bado ipo hatua za mwisho kuachia sokoni baada ya kufikia makubaliano na kampuni ya usambazaji ya Steps sasa anaingia tena msituni kurekodi filamu nyingine. Manaiki Sanga aliendelea kusema kuwa filamu hiyo ambayo itachezwa na wanamuziki kama Azonto toka nchini Uingereza na kiongozi wa kundi la Makhirikhiri toka nchini Botswana na mwanamuziki toka nchini Kenya Jaquar na hapa nchini watachukuliwa msanii Jakob Steven, Wema Sepetu, King Majuto, Lulu Michael, Zigamba na Mzee Majuto. Manaiki ambae amewahi kuitisa dunia kwa picha zake za aibu kwa wanawake zaidi ya 800 aliotembea nao tena bila kondom wakiwemo mastaa wakubwa wa bongo movie pamoja na mtoto wa familia ya Rais wa Zanzibar. Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt