TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, May 30, 2014

MAZISHI YA RECHO NA MWANAE YAACHA SIMANZI KUBWA NCHINI, MUMEWE ATAJA SABABU YA KIFO CHAKE UCHAWI WAHUSISHWA ANGALIA TAARIFA HII HAPA..!



VILIO! Vilio! Vilio! Wakati aliyekuwa mwigizaji wa sinema za Bongo, Rachel  Haule ‘Recho’ au Sheila na mtoto wake wakizikwa jana kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar huku vilio vikitawala kila kona, mumewe George Saguda ameanika mazito akihusisha kifo hicho na ulozi au uchawi kwa jina jingine.

Mume wa marehemu Saguda akilia kwa uchungu kwenye jeneza la Rachel  Haule ‘Recho’ au Sheila.
MAKABURI YA KINONDONI
Jana baada ya miili ya marehemu kuagwa Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Dar msafara wa kuipeleka kupumzishwa kwenye makaburi ulianza huku wombolezaji, wakiwemo mastaa walisikika wakisema kwamba Makaburi ya Kinondoni yanazidi kumeza mastaa katika siku za hivi karibuni kwani ukimweka kando Recho, mastaa wengine kama Adam Kuambiana, Steven Kanumba, John Maganga, Zuhura Maftah ‘Melisa’ na wengine wamezikwa hapo.

KUAGA, MAZISHI
Mastaa kibao walizimia walipojumuika kuiandaa miili ya Recho na mwanaye kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kisha kuipeleka nyumbani kwa mjomba wake Evans Haule, Sinza-Palestina, Dar ambapo familia iliaga kabla ya kwenda Leaders Club na baadaye kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Muigizaji maarufu kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rose Ndauka akilia kwa uchungu.
JENEZA LA RECHO LASHINDIKANA KUINGIZWA NDANI
Hata hivyo, jeneza la Recho lilishindikana kuingia ndani ya nyumba ya mjomba’ake kwa vile mwili ulivimba hivyo liliandaliwa jeneza kubwa ambalo halikuweza kupita mlangoni na kuishia nje tofauti na taratibu.

NJE YA MAZISHI
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Recho, katika kipindi chote cha ujauzito marehemu alikuwa akijificha kama shosti yake, Jennifer Kyaka ‘Odama’ naye alipokuwa na mimba ili kukwepa macho ya  ‘wabaya’.

AHAMA NYUMBA
Habari za uhakika kutoka kwenye chanzo chetu zinasema kuwa katika kipindi hicho, marehemu alikuwa akitokewa na mauzauza kibao hali iliyomlazimisha ahame nyumbani kwake Sinza, Dar na kwenda kuishi kwa Saguda, Kinondoni jijini Dar.

Chanzo kilisema uamuzi wa marehemu kuhamia kwa Saguda haukusaidia kuondokana na ‘madongoloji’ hayo kwani bado mauzauza yaliendelea kwa kadiri ujauzito ulivyozidi kukua.
Habari zilieleza kuwa miezi miwili kabla ya kukutwa na mauti, Recho aliamka asubuhi moja na kujikuta amechanjwa chale sehemu mbalimbali za mwili hasa kwenye mapaja kitendo kilichomshangaza sana.

MAUZAUZA LAIVU
Katika kuthibitisha hilo, marehemu alitundika picha yake kwenye Mtandao wa Instagram zilizoonesha chale hizo na kusema:

“Ya leo kali! Yaani naamka sasa hivi nakutana na hivi vitu (chale) mwilini mwangu.
“Wakati mpaka jana nalala majira ya saa nane usiku nilikuwa nipo sawa kabisa. Bado najiuliza hizi chale zimetoka wapi? Da! Eee Mungu naomba kama kuna ubaya wowote pigana na mimi (dhidi ya adui).”
Ilisemekana kwamba siku chache baadaye mambo yalimzidia akaandika tena kwenye ukurasa wake huo: “Watashindana lakini hawatashinda.”

“Kuna wakati mambo yalikuwa magumu ikabidi aende Songea (Ruvuma) kufanya tambiko kwa bibi yake, aliporudi mambo yalitulia kidogo. Nakumbuka hata ninyi (Global) mliandika habari hiyo,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kuna kipindi Recho alilalamika kwenye vyombo vya habari kwamba, kuna wasanii ambao hakuwataja majina alidai wana vijiba vya roho dhidi yake hasa mafanikio aliyokuwa akiyapata kwa kufanya kazi kwa bidii.

“Walipoona upande huo wamekwama akalalamika kuwa hawapendi uhusiano wake na Saguda ambaye ni cameraman wa muvi za Bongo. Ndiyo maana hata alipopata ujauzito hakutaka uonekane kwani alijua wabaya wake wasingefurahishwa.
USHIRIKINA BONGO MOVIE
“Huenda kweli kuna mkono wa mtu kwenye kifo cha Recho na mwanaye kwa maana Bongo Movie kwa ushirikina nao hawajambo,” kilisema chanzo.

Uchunguzi wa Ijumaa ulibaini kwamba watu wengi walikuwa hawaamini kama Recho ameaga dunia hadi walipoona jeneza hivyo kila mtu kusema lake.
SAGUDA ANASEMAJE?
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilizungumza na mumewe Saguda ambaye alisimulia mambo mazito huku akilia kukosa mke na mtoto kwa mpigo.


Kwanza Saguda alikiri kuwepo kwa mazingira ya uchawi au ‘mkono wa mtu’ kwenye kifo cha mwanadada huyo akidai kuwa mbali na kuchanjwa chale, pia kuna vitu vingi vya ajabu vilivyokuwa vikimtokea  ambavyo akivikumbuka anajikuta akimwaga machozi.
MAMBO MAZITO
Saguda alisema mambo mengine ni mazito hawezi kuyazungumza hadharani hivyo yatabaki kuwa moyoni mwake milele ila ukweli ni kwamba yeye na marehemu wamepitia katika kipindi kigumu wakati wa ujauzito huo.

KUMBE ALITAKA KUZAA MAPEMA KABLA HAJAFA
Kumbukumbu kutoka kwenye makabrasha zetu zinaonesha kuwa, Septemba 12, mwaka jana, Recho aliongea na paparazi wetu na kusema kuwa, kutokana na vifo mfululizo vya wasanii ameamua kuzaa mapema kabla hajafa ili akifa aache urithi.


Habari hiyo iliandikwa kwenye Gazeti la Amani ikiwa na kichwa kisemacho: RECHO ASAKA MIMBA (mwandishi Gladness Mallya).
Marehemu aliyasema hayo akiwa  kwenye msiba wa aliyekuwa msanii wa filamu, Zuhura Maftah ‘Malisa’ ambapo alibainisha kuwa maisha ya sasa ni mafupi tofauti na zamani hivyo bora azae haraka.
“Maisha yetu siyo marefu kama yalivyokuwa ya wazee wetu, angalia wasanii wengi waliotangulia bado ni wadogo na wengine hata hawajaacha watoto, inauma sana. Mungu akipenda nitapata ujauzito muda wowote ili nizae maana hali ni tete,” alisema Recho kwenye mahojiano hayo.

BONGO MUVI KUNA NINI?
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya mastaa wa Bongo Movie walionesha kusikitishwa na msiba huo wakisema ni mzito haujawahi kutokea kwenye tasnia hiyo kwa mama na mtoto kuondoka pamoja.


“Ukweli ni msiba mzito! Eee Mungu tusaidie, tunusuru na balaa hili,” alisema mwigizaji Steven Jacob ‘JB’.
Recho alifariki dunia Mei 26, mwaka huu baada ya kujifungua na kusumbuliwa na presha, kisukari na kifafa cha mimba.

Baadhi ya filamu alizocheza marehemu huyo ni pamoja na Danger Zone, Family Disaster, Long Hope (haijatoka), Mke Mwema, Gentlemen, Cindy, Life to Life, Loren, Men’s Day Out, Unpredictable na Figo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

ANGALIA ZIARA YA KWANZA YA VIONGOZI WA KITUO CHA RADIO 93.7 E-FM WILAYANI TEMEKE JANA NI SEHEMU YA MAANDALIZI YA MAJUKUMU YA KIJAMII JUMAPILI HII..!

 Mjumbe  kamati ya Usafi Soko la Tandika na Temeke Bw Hassan Mjaliwa akiwaonesha jambo viongozi wa ngazi za juu wa kituo hicho cha radio kinachotarajiwa kuzinduliwa Jumapili hii tarehe moja Uwanja wa Mwembe Yanga Jijini Dar.

  Bw Hassan Mjaliwa akiendelea kutoa maelekezo kwa viongozi wa radio hiyo 93.7 E-FM

 Hapa hivyo jambo la kipekee na lililoleta faraja kwa wananchi wengi ni namna viongozi hao mara baada ya kumaliza ukaguzi wa sehemu zitakazofanywa usafari Jumapili hii kama mchanga wa kituo hicho kwa jamii viongozi hao walijichanganya na wananchi kwa mama ntilie na kupiga msosi mwanzo mwisho kama picha zinavyoonesha hapa.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha 93.7 E-FM Majey anaekula ugari kushoto kwake ni Dizzo ambae ni Program Manager pamoja na Henry Mdimu pamoja na Sos Ambakise

 Mkurugenzi Majey akinawa mikono tayari kupiga msosi kwa mamantilie huko Tandika mtaa wa Ugweno na Mtandu
 Timu nzima ya viongozi wa 93.7 E-FM   Wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya Temeke pamoja na  Mh. Sophia Mjemba


PICHA ZOTE NA LIVINGSTONE MKOI

Thursday, May 29, 2014

HUU NDIYO MPANGILIO WA SHOO YA TEMEKE MWEMBE YANGA JUMAPILI HII TAREHE 1 MWEZI WA SITA KITANUKA VIBAYA..!

 JAGWA MUSIC GROUP
 MSAGA SUMU
MKUDE SIMBA
NAS B MAN BRAY

ILI KUJUA WANAMUZIKI WATAKAOTARAJIA KUPAMBA JUKWAA JUMAPILI HII TAREHE SIKILIZA 93.7 E-FM AMBAPO TAYARI WANAMUZIKI HAO WAMETAJWA

MMH ANGALIA MESEJI YA MWANAMKE ALIYEOMBA LAKI 3 ETI YA KUSUKA, MAJIBU YAKE HAYA HAPA..!



WAZUNGU BWANA ONA WANAVYOUMIZA VICHWA KILA SIKU ANGALIA HII MPYA TOKA SKYPE..!



Screen Shot 2014-05-29 at 8.59.32 AMMtandao wa skype ambao umekua ukitumika na watu mbalimbali duniani kama njia ya kuwasiliana huku kila mmoja akipata nafasi ya kumuona mwenzake wa upande wa pili kwa njia ya video, umepata kitu kingine kipya kitachorahisisha mawasiliano zaidi. (Skype Translator)
Unaambiwa kabla mwaka 2014 haujaisha, Microsoft wana mpango wa kuileta hii huduma itumike na kila mtu, yani ni application ambayo inaweza kutafsiri lugha mbalimbali na kuwawezesha watu wanaowasiliana kwa lugha tofauti kusikilizana papo kwa papo mfano mtu anaeongea Kijerumani akaongea lugha hiyo lakini wa upande wa pili akawa anamsikia kwa Kiingereza.
Wanasema hii imekuja kuvunja mipaka ya matumizi ya lugha, sasa itakuwezesha kuwasiliana na kuelewana na yeyote ulimwenguni kwa sababu inayachukua uliyozungumza na kuyaweka kwenye lugha uliyochagua, sauti inakua ileile ya kiume kama wewe ni Mwanaume au ya kike kama wewe ni Mwanamke.
Kitu kimoja ambacho sijakifahamu ni kama Kiswahili kitafanya kazi ndani yake, unaweza kutazama hii video hapa chini ili kuipata zaidi.

Wednesday, May 28, 2014

ONYO KALI, CHUNGA SANA NAMBA HIZI ZA MATAPELI WA MJINI, WAMESHAWALIZA WANANCHI WENGI JESHI LA POLISI LAWATANGAZIA KIAMA KUANZIA SASA NI KWENYE OPARESHENI YA KUKAMATA WAHALIFU UNAOENDELEA SASA..!

CHUNGA SANA NAMBA HIZI   ZASIMU ZINAZOTUMIWA NA MATAPELI JIJINI DAR NA MIKOA MINGINE..!
1.0715-426676- Huyu hujifanya yupo Rufiji fundi mkuu
2.0762-601106- Huyu hujifanya meneja wa mladi
3.0783-068678- Huyu ndiye mtafuta Tenda
4.0789-897474- Huyu anajifanya Afsa Suma JKT
Wanambinu nyingi za kumuingiza mjini mtu na tayari wameshawaibia wananchi wengi sana hujifanya wapo 
Hata hivyo taarifa zilizonaswa na blog hii zinasema kuwa Jeshi la Polisi Kinondoni limeanza msako wa chini kwa chini kuanzi tarehe ya leo 28/5/2014 ili kuwanasa watuhumiwa hawa kwani wamekuwa kero kubwa kwa wananchi.

ANGALIA KUMBUKUMBU YA KUDUMU YA MSANII RECHO KWA MASHABIKI WAKE INASIKITISHA SANA JAMANI.. KWELI MBEYE YETU NYUMA YAKE HII HAPA...!



Marehemu Racheal Haule enzi za uhai wake.



Recho ametamba kwenye Filamu nyingi zikiwemo za Miss Recho, Inside, Chocolate, Figo, Loreen, Vanessa in Dilema, Fedhea, Long hope na nyinginezo nyingi.

KUMBUKUMBU KIFO CHA MANGWEA YAZUSHA BALAA, MASHABIKI TOKA DODOMA, DAR WAMIMINIKA MKOANI MOROGORO KUSHIRIKI TAMASHA KUBWA ANGALIA TAARIFA HII..!

.
ngweaIlikua ni mchana May 28 2013 ndipo zilipotoka taarifa ambazo kulingana na ukubwa wa jina la mangwea Tanzania hakuna aliyekua tayari kuamini kama ni kweli Mangwea kafariki dunia,zilianza taratibu za kuthibitisha taarifa hizi ambapo baadae ilithibitika kweli Mangwea amefariki dunia.
Mpaka sasa ripoti kutoka hospitali ya South Africa familia haijawa tayari kuiweka wazi,kutoka Morogoro nimepata taarifa kuwa leo kutakuwa na ibada asubuhi kisha jioni kutakua na tamasha la kumkumbuka Mangwea ambapo itakua ni kumchangia mama yake Mangwea na imeandaliwa na baadhi ya wadau wa Morogoro na kupata baraka toka kwa Familia ya Mangwea.




IMG-20140525-WA0001

DUH LULU MICHAEL KIBOKO KWA SIKU ANAPIGA PICHA HAMSINI NA NGUO TOFAUTI HII HAIJAWAHI TOKEA KWA MSANII YEYOTE TANZANIA. XDEEJAYZ LIVE BILA KIG'AMUZI..!


Huyu si mwingine bali ni mdogo wetu aliekulia kwenye TV (kwasisi wa miaka ya 80 )...yaaani ana  TV personality toka LONG , kwa hapa Bongo ni staa wetu tumependwa na wengi (pamoja na mimi toka kitambo) anaitwa Elizabeth Michel  a k a Lulu...Ameibuka na kusema kila siku iendayo kwa Mungu anapiga picha zaidi ya 50 na nguo tofauti  hali iliyofanya avunje rekodi na kuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo Tanzania ameieleza Xdeejayz Tanzania.
CHANZO: XDEEJAYZ TANZANIA

MAAJABU YA DUNIA, ALIYETAKA KUMBATIZA MWANAE JINA LA YESU APINGWA DUANIA NZIMA ANGALIA TUKIO HILI LA KUSHTUA..!


Ndiritu Njoka kwenye headlines tena wakati huu sio kukabiliana na Wanawake wanaowapiga Waume zao bali wakati huu jamaa anataka kanisa na Presibiteria ya Africa Mashariki-PCEA kumbatiza mwanae wa kiume aliempa jina la Jesus ama Yesu.
Njoka amesema ameamua kumpa mwanae jina hilo kwasababu jina Yesu ni jina zuri sana >>’Sijamuita mwanangu kristo, nimemuita Yesu kwasababu ni jina nzuri sana’
Njoka pia amedai kwamba kanisa na hata hospitali aliyozaliwa mwanae wamekataa kumuandikia cheti cha taarifa ya kuzaliwa kwasababu hawataki kuandika Jina Yesu kwenye cheti hicho.
Njoka alipoulizwa kuhusu hilo amesema >>’hata kama hospitali walikataa kuandika hilo jina Yesu, nitatumia mkono wangu kuandika hiyo taarifa ya kuzaliwa Yesu Njoka kwasababu huyo ni mwanangu’.
Rais huyo wa Wanaume ambae amekua akihusika na chama cha kutetea haki za Wanaume duniani ameongeza kuwa ameacha kwenda kanisani kwa sababu ya kukataa kumbatiza mwanae Yesu >’nimewaambia sawa basi hata hayo mambo ya kanisa nitaacha na nitakua nikiomba nyumbani kwasababu kama shida ni kumwita mwanangu yesu si lazima niende kanisani’
Screen Shot 2014-05-28 at 2.25.36 PMNae katibu mkuu wa kanisa hilo la PCEA Kasisi Thegu Mutahi anasema jina la Yesu hawezi kupewa mtu maana Yesu ni mwana wa mungu >>> ’ukimuita mtoto yesu unamwona hapo barabarani akicheza na wenzake anaitwa Yesu !, Yesu !, Yesu ! hilo jina na tunajua yesu ni mwokozi litachukuliwa vipi?’.
Aidha Njoka amesema amekerwa na hatua ya kanisa kukataa majina mazuri wakati wananyamazia watu wanaojiita Mwashetani na wengine Mwakaburi ambapo kwa sasa Njoka amesema amemuandikia barua Papa wa kanisa Katoliki kama njia ya kutafuta kibali kumuita mwanae Yesu Njoka Njoka.

JESHI LA POLISI LATANGAZA KIAMA KWA WATOTO WA MBWA, MSAKO WA MTAA HADI MTAA UMEANZA JANA MAENEO YA YOTE YA JIJI LA DAR..!


Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.
 Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.  Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita

KIFO CHA RECHO, STEVE NYERERE ALIA HADI KUPOTEZA FAHAMU ANGALIA TUKIO HILO HAPA XDEEJAYZ TANZANIA




Monday, May 26, 2014

KUMEKUCHA IJUMAA HII NI BALAA TUPU NDANI YA CLUB MAISHA DAR NI USIKU WA TATOO KAMA WEWE UNATATOO ZA AJABU FIKE UJICHUKULIE ZAWADI BAB KUBWA ANGALIA HAPA..!


HATARI KUBWA, WAZARAMO NA WATANGA KUTOANA ROHO JUMATANO HII NDANI YA CLUB MAISHA DAR NI KWENYE USIKU WA BUNYEROBUNYERO NI BALAA TUPU HAIJAWAHI TOKEA..!


TIZAMA TUKIO LIVE LA WIZ KHALIFA ALIPONASWA NA MISOKOTO YA BANGI 200 AIRPORT PALIKUWA HAPATOSHI.. XDEEJAYZ LIVE..!

s
Screen Shot 2014-05-26 at 2.13.17 AMStaa wa hiphop kutoka Marekani Wiz Khalifa (26) Jumapili ya May 25 2014 amedakwa na polisi katika uwanja wa ndege huko Texas Marekani baada ya kukutwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi kwenye mizigo yake zipatazo 200.
Alikuwa akisafiri kutoka El Paso kwenda Dallas wakati maafisa wa uwanja wa ndege walipokuta mzigo huo ndani ya begi lake ambapo kwa mujibu wa sheria aliwekwa kizuizini na baadae kufikishwa kituo cha polisi kabla ya kuachiwa huru saa kadhaa baadae kwa mujibu wa TMZ.
Screen Shot 2014-05-26 at 2.04.49 AMPamoja na hayo, yeye mwenyewe Wiz hakuonyesha kujali ambapo baadae alitweet picha yake akiwa chini ya ulinzi na kuonyesha hiyo ishu haijamsumbua akili kabisa.
Alipokua chini ya huo ulinzi kwa saa kadhaa Khalifa alitweet na kuonyesha picha zake akisisitiza pia kuachiwa huru.
Screen Shot 2014-05-26 at 2.13.55 AMScreen Shot 2014-05-26 at 2.14.06 AMHiyo ndege binafsi ya kusafiria kwenye picha ya kwanza hapo juu  ndio inaaminika aliitumia kusafiri muda mfupi baada ya kuachiwa huru na kupiga picha akiwa pembeni yake kuthibitisha kwamba aliachiwa huru.
Alipoulizwa na shabiki wake kama alipata mateso yoyote alipokua chini ya huo ulinzi, Khalifa alijibu kwamba kila kitu kilikua poa, yani alikaa vizuri tu bila matatizo.
Staa huyu aliefanya mpaka bongo imfahamu kwa sana kupitia single yake ya ‘Black and Yellow’ hii ni mara yake nyingine kukamatwa na bangi ambapo kisa kingine kilitokea November mwaka 2010.

ANGALIA VITUKO VYA NDOA YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN JANA, ILIKUWA BALAA TUPU BEYONCE AWA WA KWANZA KUPOST PICHA HIZI...!


article-2638252-1E26AF4500000578-868_634x565
Kim Kardashian amekuwa Mrs. West rasmi leo baada ya kufunga ndoa na Kanye West.Mastaa hao wamefunga pingu za maisha kwenye harusi private iliyofanyika juu ya mlima Fort di Beleverdre huko Florence, Italia mbele za ndugu na marafiki zaoHata hivyo marafiki wakubwa wa Kanye, Jay Z na mke wake Beyonce hawakuwepo kwenye harusi hiyo.
Awali ilisemekana kuwa Jay Z angekuwa mpambe wa Kanye kwenye harusi hiyo kwakuwa wawili hao ni marafiki wa karibu. article-2638252-1E2BCD2D00000578-859_634x605Beyonce alipost picha hii muda ambao Kanye na Kim walikuwa wakifunga ndoa

WEMA, AUNT EZEKIEL CHUPUCHUPU KUBAKWA ANGALIA TUKIO HILI LA KUSHTUA ILIBAKI KIDOGO TU JAMAA ANANIHII...!


Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwa katika Msiba wa Adam Kuambiana.
Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walikipata cha moto walipokuwa kwenye msiba wa Adam Kuambiana, Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar, baada ya kutukanwa na njemba mmoja aliyekuwa amelewa.
Sakata hilo lilijiri usiku mwingi wakati  mastaa hao walipokuwa wameenda kulala kwenya matanga ambayo yalihudhuriwa na mastaa kibao, nyumbani kwa mke wa marehemu
Mwanaume mmoja (jina lake halikupatikana) alianza kumtukana Wema kuwa hana uzuri wowote kama walivyokuwa wakimuona kwenye runinga.
Kitendo cha njemba huyo, kilimkera Wema na kuanza kujibishana naye, Aunt akaununua ugomvi na kujikuta naye akitemewa mbofumbofu.
Hata hivyo, mwisho wa sakata hilo Wema na Aunt waliamua kunyamaza kwani walibaini kuwa walikuwa wakijibishana na mtu ambaye ‘network’ yake ilikuwa bize kwa gambe.