TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, January 31, 2013

NYIMBO ZA MWANAMUZIKI MANAIKI SANGA KUMPATIA MAMILIONI YA SHILINGI!

 Mwanamuziki nyota wa bongo flava nchini Manaiki Sanga
Manaiki Sanga.
Na Livingstone Mkoi
Nyimbo za mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipy nchini Manaiki Sanga zimeinginzwa kwenye mtandao kwa ajili mashabiki kupta fulsa ya kuzisikiliza kupita simu zao za viganjani.
Akiongea na Xdeejayz Manaiki ambae mwaka jana alitamba sana na nyimbo zake kali kama Nina fanya mambo na nyinginezo na kufanikiwa kusimama kwenye top ten mbalimbali za kwenye redio na tv.

Manaiki alizitaja nyimbo alizoziingiza kwenye mtandao na namna ya mashabiki wake watakavyoweza kuzipata ambao:CODE ya wimbo na Nafanya Mambo ni 21849. Na CODE  ya wimbo Twende Sawa ni 21809. nyimbo zote hizo unatumakwenda namba 15007.

Maelekezo mengine ni unaenda sehemu ya kuandikia sms na kuandika unachagua wimbo unaoutaka kwa namba iliyoelekezwa hapo juu kisha unatuma kwenda namba 15007.

Aidha mwanamuziki huyo aliongeza kusema wimbo wa nafanya mambo ambao aliwashirikisha mastaa kibao kama vile Maunda Zoro,Mr Blue, Godzila nk anampango wa kuutengenezea filamu na tayari ameshawaita mastaa kibao wa filamu nchini akiwemo Mzee Magali ili kujipanga.

UKIMWI WATEKETEZA MAMIA YA WAHUDUMU KITUO CHA MABASI UBUNGO!

 Mkusanyiko wa watu kama huu ndani ya  kituo cha mabasi Ubungo umedaiwa kuongeza maambukizi hatari ya ugonjwa wa ukimwi.
 Eneo la kituo cha mabasi Ubungo kama kinavyoonekana.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh John Mnyika.
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushtua kumeibuka taarifa za kutisha juu ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa ukimwi yanayoendelea katika kituo cha mabasi cha Ubungo kwa sasa.

Xdeejayz ifunga safari hadi kutuoni hapo baada ya kutonywa na baadhi ya wahudumu wa kituo hicho na kusikitishwa na mienendo ya maisha ya vijana yanavyokuwa hatarini.

Wakiongea na mwandishi wetu kituoni hapo kwenye mahojiano maalum wahudumu hao walisema kuwa ki ukweli hali ya maisha ya  vijana kwenye kituo hicho ni mbaya sana kwani  kwani kila kukicha kunaibuka maambukizi mapya.

Mmmoja wa akina dada ambae ni muhudumu wa kituo hicho alianza kusema" Kaka hali ni mbaya kwa kweli hapa Ubungo kuna nuka ngono ukimwi unatekekeza vijana hasa hawa maajenti wengi wameathirika sana hivyo kuna mzunguko mkubwa sana wa maradhi hayo hapa, na inatakiwa juhudi za haraka kuchukulwa ili kuwanusuru vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa" Alisema Dada huyo ambae aliomba hifadhi ya jina lake

Hata hivyo dada huyo aliendelea kusema" Mara nyingi maajenti wengi wanaponzwa na tamaa kwani kuna wafanyabiashara wa kila aina hivyo wakija kama kuchukuwa tiketi kisha humuachia hela ya soda kama laki hapo ndipo hunaswa kwani hufikiri kuwa kama soda tu kampa laki je akitembea nae si atampa mamilioni ya fedha" Kilisema chanzo hicho
Baadhi ya watu katika soko hilo wametoa uwito kwa mbunge Jimbo hilo ndugu John Mnyika kufanya jitihada za kuwaelimisha vijana hao la sivyo miaka kumi mbili hali itakuwa mbaya kwani kwa sasa kinachofanyika ni kuambukizana makusudi tu wenyewe kwa wenyewe.

MBWANA MATUMLA ANAOGOPA KUPAMBANA NA MIMI TENA:FRANCIS MIYEYUSHO

Bingwa wa Dunia WBF,UBO Mtanzania Friancis Miyeyusho

Na Livingstone Mkoi
Bingwa wa mabara wa dunia nchini Francis Miyeyosho ameibuka na madai kuwa bondia Mbwana Matumla anamuhofia kupigana nae kwa vile kiwango chake kwa sasa kimeshuka sana.
Akiongea na Xdeejayz ndani ya gym yake iliyopo Kinondoni Mkwajuni Miyeyusho alisema kuwa kwa sasa nchini hana mpinzani kwa vile kesha wapiga mabondia wote hivyo anasubiri pambano lake  na bondia toka Ufilipino ambalo litafanyika hapa nchini mwanzoni mwa mwezi wa tano.

Miyeyusho ambae hivi karibuni alimtwanga kwa KO bondia Nassibu Ramadhani  na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa WBF na kufanikiwa kumiliki mikanda miwili baada ya ule wa UBO ambao aliuchukuwa kwa Mbwana Matumala baada ya kumuadhibu kwa kipigo kikali.

Wednesday, January 30, 2013

NEW SONG (AUDIO) by SNURA - MAJANGA

http://www.hulkshare.com/f4p75h1d9kw0 SIKILIZA MZIGO MPYA WA SNURA - MAJANGA

Halafu jumapili hii tukutane new mausha club kwenye VIUNO SHOW hii sio yakukosa kabisa kiingilio elfu 8 tu wasanii kibao watamsindikiza,PNC,DOGO JANJA,PASHA,TUNDA MAN,RICH MAVOCO,Y TON MIRROR,NUH DA STAMINA,SCOPION GALZ NA WENGINE KIBAO.

KILI XTREME DEEJAYZ KUWASHA MOTO KWENYE LADIES NIGHT NEW MAISHA CLUB DODOMA ALHAMISS HII

 Baada ya kufanya poa mtwara na dar es salaama wale wakali wa madeejayz tanzania KILI XTREME DEEJAYZ Alhamisi ya leo wapo NEW MAISHA CLUB dodoma kutoa burudani kali . Huku mashabiki watarazimika kuchangia mchakato kidogo tu wa  buku 5000/= Mlangoni kwa akina kaka na akina dada wataingia bureee kabisa bila bughuza.

DVJ MAJEY na HYPERMAN HK wamesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanawapa burudani zote kali wakazi wa mjii wa dodoma na vitongoji vyake ,mashabiki wameombwa wajitokeze kwa wingi kuja kuona mambo ya KILI XTREME DEEJAYZ. 

BAMBO AUGEUKIA MUZIKI WA INJIRI, AINGIA STUDIO!

 Dickson Samsoni Makwaya a.k.a Bambo

Na Livingstone Mkoi
Msanii nyota wa maigizo nchini Dicksoni Samsoni Makwaya a.k.a Bambo ameingia studio kurekodi muziki wa injiri akiwa na mchungaji maarufu nchini.
Akiongea na Xdeejayz juzi Bambo alisema alifatwa na mchungaji Leonard Gaspa wa kanisa TAG Mkoani Mwanza na kumtaka kushirika kwenye wimbo wake mpya ambapo alikubari.
Bambo aliongeza kusema kuwa wameshaingia studio tayari na wamekamisha kurekosi wimbo huo unataitwa Tumekuwa Wakiristo.

WAHESHIMIWA WABUNGE,TRIPLE BASH KUACHA HISITORIA NDANI YA MAISHA CLUB DODOMA IJUMAA HII!

HEMED KAVU (HK) A.K.A HYPERMAN

Na Livingstone Mkoi

Wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake Ijumaa ya wiki hii wanatarajia kupata kushuhidia shoo ya kijanja itakayofanyika ndani ya Maisha Club, huku waheshimiwa wabunge mbalimbali wakitarajia kuhudhuria shoo hiyo.

Akiongea na Xdeejayz kwa njia ya simu toka Dodoma mratibu wa shoo hiyo toka kamapuni inayoongoza kuambukiza virusi vya burudani tanzania ya Entertainment Masters Ltd Hemed Kavu a.k.a Hyperman alisema"Tuna malizia mzunguko huu wa Triple Basha kwa mfumo wa ONE DJ ONE SHOW THREE VENUES kwa Maisha Club ya Dodoma baada ya shoo kama hizi kufanyika kwenye Club zetu za Mtwara na Dar es Salaam" Alisema HK

Aidha mratibu huyo aliendelea kusema kuwa maandalizi yote yamekamilika ambapo timu ya maangamizi kwa ajili ya kutoa burudani imeshaingia Mkoani humo ikitokea Dar na cha kuvutia kwenye shoo hiyo ambacho ni kama "surprise" kwa mashabiki ni uzinduzi wa mashine mpya ainanya Pioneer" Alisema maratibu huyo

Hata hivyo kivutio pekee kwenye shoo hiyo ni Dj nyota Afrika Mashariki  ambae ni kipenzi cha watu wengi Dj Majay a.k.a Majizo 4 Jizo anatarajia kuwahenyesha mashabiki hao kwa upigani wa mfumo wa DVJ mtindo ambayo Club Maisha uliunzasha nchini na baadae kuigwa sehemu mbalimbali.

HK alimaiza kusema kuwa pia wanatarajia kuwaalika Waheshimwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iki kuja kupoza akili zao kwa burudani hiyo kwani tarayi itakuwa mwisho wa Juma siku ambayo watakuwa mapunziko.

Tuesday, January 29, 2013

BLOG YA XDEEJAYZ YATIKISA NCHINI AFRIKA KUSINI,MTANGAZI WA AFRIKA MAGIC SWAHILI KUINGIA NAYO UBIYA WA MATANGAZO!

 Mtangazaji ambae ni mtanzania anayetangaza Afrika Magic Swahili, nchini Afika Kusini  Fortunatus Kasomfi akiwa picha ya pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu.

Fortunatus Kasomfi

Na Livingstone Mkoi
Mtangazaji nyota wa Radio Afrika iliyopo nchini Afika Kusini ambae nia ni ripota wa Afrika Magic Swahili Fortunatus Kasomfi amesema anamikakati ya kuingia mkataba  wa kufanyakazi na blog hii inayoongoza kwa sasa kuwa na wasomaji kwa vile imekuwa blog pekee inakubarika nchini Afrika Kusini.

Fortunatus ambae pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Forjoys Art Production Inc yenye makazi yake Johannesburg  aliendelea kusema kuwa licha ya nchi ya tanzania kuwa na utitili wa blogs lakini watanzania wengi waishio nchini Afrika Kusini hupenda sana kutembelea blog ya xdeejayz kutokana na kuwa na habari za uhakika pamoja na picha matukio ya kusisimua.
Aidha mtangazaji huyo ambae kwa sasa yupo nchini Ujerumani kikazi na mwisho wa mwezi ujao atarejea nchini Afrika Kusini kisha kurudi nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa blog hii ambao ni kampuni ya  Entertainment Masters Ltd
Hata hivyo Fortunatus alimaliza kusema kuwa kutokana na kampuni yake kushughulika na mambo ya sanaa hivyo itakuwa njia nzuri kwa kufanya kazi pamoja na xdeejayz ambayo kimsingi imekaa kiburudani zaidi pamoja na habari.

MWANAMUZIKI ALEX WA MACHEJO ANUSURIKA KUULIWA,WANANCHI WENYE HASIRA WAMJERUHI VIBAYA !

 Mwanamuzi wa bongo flava Alex Machejo akiwa na baadhi ya wasanii wa komedi


 Alex Machejo akiwa nyumbani kwa bibi yake mwananyama Jijini Dar akijiuguza pichani kama anavyoonekana siku alipotembelewa na mwandishi wa Xdeejayz


Na Livingstone Mkoi

Katika hali ya isiyokuwa ya kawaida na kusikitisha mwanamuziki nyota wa bongo flava Alex wa Machejo hivi karibuni alinusurika kuuliwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutupiwa mdudu.

Habari za uhakika toka kwa mwananmuziki huyo zilisema kuwa ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu akiwa nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni Moscow Jijini Dar es Salaam usiku ghafla alisikia kizunguzungu pamoja na kiza nene machoni mwake kisha akadondoka.

Hata hivyo hali hiyo aliichukuliwa kama ni kawaida tu.Lakini cha ajabu hali hiyo haikumuacha hadi siku iliyofuata ambapo sasa mambo yalibadilika ambapo akaanza kupiga kelele kama mtu mwenye kichaa.

Mwanamuziki huyo aliendelea kusema kuwa alianza kukimbia ovyo  huku wananchi wakimuungia kwa kupiga kelele za mwizi pamoja na kuanza kumpiga kwa mawe na nondo kichwani.

Lakini hata hivyo baadhi ya watu wanaomjuwa mwanamuziki huyo walifanikiwa kumuokoa mikononi mwa wananchi wenye jazba kali kwa kumtetea kuwa hakuwa mwizi bali anaumwa.

Alex aliiambia xdeejayz kuwa hafahamu ni kwa nini watu wabaya waliamua kumfanyia hivyo kwani uchunguzi umebaini kuwa alitupiwa mdudu mbaya na bila nguvu za mungu ilibidi afe kwa kipigo cha wananchi au awe mwendawazimu.

Timu ya waandishi wa xdeejayz inampa pole mwanamuziki huyo na mungu amjalie arudi kwenye hali ya kawaida ili kuweza kuendelea na majukumu yake ya sanaa kwa ajili ya ujenzi wa taifa.



Monday, January 28, 2013

SNURA NA SHILOLE WAFUNIKANA DAR LIVE


Ilikuwa raha sana kiukweli show ilianza kwa shilole kufanya yake baaadae snura nae aliingia kufanya yake kiukweli ilikuwa raha sana. JUMAPILI HIII USIKOSE PALE NEW MAISHA CLUB snura atafanya yake kuzindua ngoma yake mpya ya majanga.atasindikizwa na wasanii kibao kama rich mavoco,tunda man,y tony ,scopion galz,na wengine kibaoooooo kiingilio 8,000. tu










































TOUR YA TIMU YA DAR LEOPARD CLUB ILIVYOCHENGUA MKOANI IRINGA MWISHONI MWA JUMA!





Watoto washabiki wa mchezo wa rugby wakipiga picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Dar Laopard ya Jijini Dar iliyokuwa nchini Zambia na Mkoani Iringa.






 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Dar Leopard Club wakiwa katika picha pamoja siku ya Jumamosi Mkoani Iringa kwenye mashindano ya mchezo wa Rugby yaliyopewa jina la Southern Highland "Touch Rugby



 Mmoja wa wachezaji nyota wa timu hiyo ambae pia ni mwandishi wa blog hii Livingstone akiwa hoi uwanjani baada ya mchezo mkali.



 Ilikuwa ni misosi ya kitasha tu sio ugali au wali hapa ilikuwa Mabaga,Mapizza nk kama ilinayoonekana pichani.

 Hapa baada ya mechi ilikuwa ni kunywa maziwa mtindo mmoja kwani wadhani wa mashindano hayo ambao ni IRINGA ASAS DAIRIES walimwaga maziwa kama maji siku hiyo.

Hapa winga hatari wa timu hiyo akiwa ameuchapa usingizi baada ya safari ndefu pamoja na kula gambe za kutosha.

 PROP hatari wa timu ya Dar Leopard Livingstone Mkoi akiwa amepunzika kwenye Hotel ya kitalii waliyofikia wachezaji hao nje kidogo ya mji wa Iringa



 Hapa ni eneo la Mbuga za wanyama Mikumi kuna nyama za mbuzi za kumwaga pamoja nyama za wanyama poli timu ilishuka kwa ajili ya kula nyama.

 Hawamu Juma mwenye jezi ya misitari nyekundu na nyeusi akitafuna  nyama kwa hasina huku pembeni akiwa na mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.


 Mawinga hatari wa Dar Leopard kulia ni Hawamu Juma kushoto Jeremiah wakiwa wameuchapa usingizi ndani ya gari.Wakati timu hiyo ikitokea Zambia kuja Iringa

CAPTAIN wa timu ya Dar Leopard Geog Mtefu akijichagulia vipaja.Mbuzi hao ambao huuzwa kati ya shilingi elf kumi na elf nane.

Na Mwandishi Wetu 

Timu ya mchezo wa Rugby ya Dar Leopard ya Jijini imewasili leo asubuhi kwa ndege ya Flightlink ikitokea Mkoani Iringa kulikokuwa na mashindano ya Rugby kwa timu tofauti.

Akiongea na xdeejayz mmoja wa wachezaji wa timu hiyo Hawamu Juma alisema kuwa timu yao iliondoka Ijumaa iliyopita na kutua nchini Zambia na baadae kuja Mkoani Iringa kwa ajili ya kukamilisha ziara yao ya kimchezo.

Ambapo timu ambayo iliondoka ikiwa na wachezaji wote nyota ambao walionesha uwezo wa hali ya juu na kuwaduwaza wazungu ambao walishindwa kuamini kama wachezaji hao ni watanzani au laa.

Hata hivyo baadhi ya wachezaji waliofanya vyema kwenye mashindano hayo ni pamoja Hawamu Juma, Livingstone Mkoi, Jeremial,Georg Mtefu, Erika Mura,Alfonce nk.

Kwa mujibu wa captein wa timu hiyo Georg alisema timu hiyo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa hivyo Ijumaa hii itaendelea na mazoezi makali kwenye uwanja wao wa nyumbani wa IST ya Masaki.